22.11.13

Sunday, May 19, 2013

(Cheka na KITIME) ANACONDA KUMPA KIJITI ANANENEPA

Watafiti makini wa hii blog isiyo makini ambayo inakoelekea ni wazi kubaya maana maelfu ya wasomaji wa blog hii iko siku watagoma kabisa kusoma chochota kilicho humu labda wawe wanalipwa kwa dola, watafiti wamegundua kitu ambacho ingekuwa blog nyingine ingejipendekeza na kuziita BREAKING NEWSSSSSSS. Yaani watafiti wa blog hii ni kiboko, mi mwenyewe Rais wa blog hii nimewavulia kofia. Baada ya wiki kadhaa kusikia mwanamuziki maarufu Binti Machozi akiwa na sifa mpya ya kuitwa ANACONDA, watafiti waandishi wetu, wamegundua msanii mwingine ambaye yeye anajiita ANANENEPA. Msanii huyu ambaye si mpya kabisa amepewa jina hilo na mamia ya watu waliogundua kuwa amekuwa habaniwi nyimbo zake, na amekuwa anapata kazi nyingi sirikalini , ambako mwenyewe amesema zinatokana na rushwa. ANANENEPA ambae ametamba kuwa ni msanii ambaye ameenda Ulaya kuliko Mtanzania yoyote duniani, pia ameunga mkono watu kupewa vijiti, hasa kwa kuwa amekuwa anapata tabu sana kupata vijiti baada ya kula nyama.. Ngoja tuachie hapa maana ANANENEPA ametishia kwenda Mahakamani kama tutaendelea kuandika habari zake. Na ukichukulia hata jana alienda Mahakamani kusikiliza kesi mbalimbali, na Jumapili alienda Mahakamani kuangalia majengo tusingependa aende tena huko....

No comments: