22.11.13

Sunday, May 26, 2013

(News) MARTIN FUNDI NDIYO THE VODACOM MIC KING

 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akimwelekeza namna ya kuwasha gari,Bw.Martin Fundi mara baada ya kuibuka mshindi wa The Vodacom Mic King na kukabidhiwa gari hilo  na Meneja matukio wa ukumbi wa Dar Live Abdallah Mrisho hayupo pichani,Shindano hilo lilidhamini na Vodacom Tanzania.


 Meneja wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu pamoja na Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho(katikati) wakimfungulia gari mshindi wa The Vodacom Mic King 2013, Martin Fundi,mara baada ya kuibuka kidedea katika shindano hilo,Shindano hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.

 Meneja wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa The Vodacom Mic King 2013, Martin Fundi,mara baada ya kuibuka kidedea katika shindano hilo lililodhamini na Vodacom Tanzania.Katikati ni Meneja Matukio wa ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho.

 Mshindi wa shindano la The Vodacom Mic King,Martin Fundi akichana kwa hisia kali mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo huku Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akimshuhudia.Shindano hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.

 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu(kushoto)na Mshindi wa The Vodacom Mic King Martin Fundi wakifurahia kwa pamoja mara baada ya mshindi huyo kutangazwa,Shindano hilo lilifanyika Dar Live hapo jana na kudhamini na Vodacom Tanzania.

 Hii ni sita bora ya The Vodacom Mic King

 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Fid Q na Stamina wakichana vilivyo katika ukumbi wa Dar Live wakati wa kumtafuta mshindi wa The Vodacom Mic King ambapo Bw.Martin Fundi aliibuka kidedea na kuzawadiwa gari,shindano hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Joe Makini akipagawisha vilivyo katika ukumbi wa Dar Live wakati wa kumtafuta mshindi wa The Vodacom Mic King ambapo Bw.Martin Fundi aliibuka kidedea na kuzawadiwa gari,shindano hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.

1 comment:

Anonymous said...

Wat a fantastic perfomance from Mwamba wa kaskaziniiiii