Msanii
mahiri wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA ambae ni
Balozi wa Chapa Vodacom amesema hadhi na heshima ya mwanaume katika
jamii itakuwa
na uzito mbele ya uso wa jamii kwa wao kuwa tayari kutafuta suluhu ya
changamoto zinazoikabili jamii na wala si vinginevyo.
Balozi
huyo maarufu kwa jina la Mwana FA ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati
wa kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu fistula iliyofanyika katika
viwanja vya Nyerere
Square kuelekea siku ya fistula dunaini Mei 23. Kampeni hiyo
inadhaminiwa na kampuni ya Vodacom na Vodafone ya Uingereza ikiihusisha
mikoa mbalimbali.
Balozi
huyo amesema ni wazi kwamba wanaume wamekuwa wamiliki wa maamuzi katika
jamii huku wakitajwa kuwa nguzo ya familia lakini sifa hizo na mamlaka
hayo yatakuwa
na dosari kubwa iwapo hawatokuwa pia mstari wa mbele katika kuhakikisha
jamii inapata suluhisho la matatizo.
Balozi
huyo ambae alikuwa akielimisha wakazi wa mji wa Dodoma kuhusu fistula,
amesema fistula sio tatizo kama ambavyo inaweza kufikiriwa kwa kuwa
jambo gumu lingekuwa
namna ya kupata matibabu na uwezo wa kugharamia matibabu hayo.
“Hakuna
mwanamke ambaye anapata fistula bila ya mwanaume kuwa chanzo kwa kuwa
ndio tunaowapa ujauzito wake zetu, hivyo sio vema na haki kwa mwanaume
kumkimbia
mkewe au kumtenga mwanamke eti tu kwa sababu mwanamke huyo ana tatizo
la fistula.”Alisema Balozi huyo
“Nawaomba
sana wakazi wa Dodoma hasa wanaume tubadili mtazamo tulinao juu ya
fistula kwa kutambua kwamba sisi ndio chanzo cha wanawake kupata fistula
lakini zaidi
ni kwamba hilo sio tatizo kwa kuwa tatizo ni lile ambalo halina
suluhisho, fistula inatibika na tena inatibika bila malipo kwa ufadhili
wa Vodacom na Vodafone, nini zaidi tunachohitaji katika hili?.”Alihoji
Mwana FA
Amesema
uamuzi alioufanya kukubali kutembea nchi nzima kuhamasisha akina baba
kuondokana na dhana hasi juu ya fistula ikiwemo kuhusisha tatizo hilo na
ushirikina
au laana na hivyo kuwakimbia wake zao au kushiriki kwa namna yoyote
katika kuwanyanyapaa wanawake wenye tatizo la fistula ulikuwa ni mgumu
lakini alikubali kwa kuwa anaamini jamii itamuelewa.
“Haikuwa
kazi rahisi kwangu kukubali kuongoza msafara huu lakini baada ya
kutathmini na kuona jinsi akina mama wanavyoteseka kwa tatizo hili
nilijihisi mwepesi
kukubali kuzunguka kila kona kuongea na wanaume wenzangu kuwahamasisha
kuwa tayari kwa pamoja kuunga mkono kampeni hii ili kufikia lengo la
Vodacom la kumaliza tatizo la fistula ifikapo mwaka 2016 .”Aliongeza
“Iwapo
kuna mtu(Vodacom)amejitolea kutoa suluhisho la tatizo kwa kulipia
nauli, chakula, malazi na matibabu hatuwezi tena kusema fistula ni
tatizo,kikwazo pekee
tulichonayo hapa ni kuhakikisha kila mmoja anafikiwa na taarifa na
ujumbe huu.”Aliongeza
Mwana
FA amekuwa chachu katika kampeni hii kwa namna ambavyo ushawishi wake
umewezesha kwa kiasi kikubwa ujumbe wa fistula kuwaingia wanaume huku
baadhi yao wakimuahidi
kumuunga mkono kwa dhati.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy
Mwalimu alisema si haki kuendelea kuwaacha wanawake wakiteseka wakati
fursa ya kuwawezesha
kupata matibabu ipo na hivyo ameitaka jamii kuiunga mkono kampeni hiyo
na kuitumia ipasavyo.
“Tunaishukuru
Vodacom kwa kuweka mfumo wezeshi kwa jamii kupata elimu ya fistula na
pia kuwawezesha wanawake kupata matibabu ya fistula bila malipo, naomba
wakazi
wa mji wa Dodoma na nchi nzima tuitumie fursa hii na tuwe mabalozi kwa
wenzetu.”
“Vodacom
inafanya kazi kubwa sana kusaidia jamii hapa nchini. Kamwe hatutoona
aibu kuipongeza ndani na nje ya Bunge kwa kazi hiyo kubwa na znuri
wanayoifanya ikiwemo
kampeni hii ya fistula na ufadhili inaotoa kwa wanawake kupata matibabu
bila malipo.”Alongeza Ummy
Amesema
kuwa jamii lazima ione na kutambua kuwa mwanamke ana wajibu wa kuwa na
afya njema ili nae aweze kushiriki katika shughuli za kijamii na za
kiuchumi na
hivyo kuchangia maendeleo ya kaya na jamii anamoishi.
Naibu
Waziri huyo amekiri kuwepo kwa hali ya unyanyapaa kwa jamii kwa
wanawake wanaokabiliwa na matatizo ya fistula hali ambayo amesema ni
lazima ibadilike hasa
wakati huu ambapo fursa za matibabu bila malipo zipo ikiwepo na kuahidi
kuibeba ajenda hiyo kwa nguvu zake zote.
Vodacom hutumia wastani wa Sh 700,000 hadi 900,000 kulipia matibabu ya mgonjwa mmoja wa fistula kwenye hospitali ya CCBRT.
Nae
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Said Mtanda
amesema anatambua vema tatizo la fistula na athari zake kwa wanawake
wazazi na kwamba
pamoja na ukweli kuwa amekuwa akichukua juhudi binafsi katika kusaidia
wanawake wenye fistula lakini sasa anaibeba kampeni hiyo na kuiwasilisha
katika kamati yake ili kuipa nguvu rasmi za kibunge.
“Naahidi
kuwa nitawasilsiha kwenye kamati yangu ujumbe wa kamati hii ikiwa ni
pamoja na kuiomba nguvu za kamati hiyo na kuwashawishi wajumbe kuubeba
ujumbe wa
kampeni hii ndani ya Bunge ikiwemo wakati wa shughuli rasmi za kamati
na Bunge kwa ujumla.”Alisema Mtanda
Kampeni hiyo iliyolenga kuifikia mikoa mbalimbali itamaliza safari yake Mei 23 jijini Dar es salaam siku ya fistula Duniani.
Mwisho.
1 comment:
That's true
Post a Comment