Kama kamati tunaomba kutoa taarifa kwamba mwili wa Ndugu yetu Albert
Mangwea utafika siku ya jumapili ya tarehe 2/06/2013 saa nane mchana na
sio siku ya jumamosi kama ilivyotaarifiwa hapo awali , Sababu za Mwili
wa Albert Mangweha kushindwa kufika jumamosi kama ilivyopangwa ni
kutokana Watanzania wenzetu waishio Afrika Kusini kuomba na wao kutoa
heshima zao za mwisho . Kwa Maana hiyo
basi taratibu zote za kuaga mwili wa Albert Mangweha kwa Wakazi wa Dar
es Salaam na maeneo ya Jirani zitafanyika siku ya Jumatatu ya tarehe
03/06/2013 kuanzia saa mbili asubui mpaka saa sita mchana , ambapo
baada ya hapo safari rasmi ya kuelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi
itaanza. Tunaomba radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza Asante
No comments:
Post a Comment