Sindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mwanza, linatarajiwa kufanyika June 14 katika viwanja vya Yatch Club jijini Mwanza.
Warembo
18 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wamejitokeza kushiriki
shindano hilo la aina yake huku....Burudani inayosubiriwa kwa hamu kubwa
ni Mh. Mbunge Joseph Mbilinyi maarufu kama sugu atakapo panda jukwaani
kukumbushia enzi hizo...akishindikizwa na mkali mwingine wa Chege
Chigunda kutoka TMK.
Warembo wote wanatarajiwa kuanza kabi rasmi
Jumanne hii katika moja ya hoteli maarufu jijini humo.
Itakumbukwa mkoa wa Mwanza
tayari ulishatoa Mrembo wa Tanzania, ambaye ni Nasreem Karim 2009 na
Miriam Gerald 2010. Pamoja na mchakato wa shindano la urembo kuendelea
kwa hivi sasa nchini, macho na masikio yapo mkoani Mwanza, ambako
kumekua kukileta changamoto na upinzani mkali wa warembo kila Mwaka.
No comments:
Post a Comment