Tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa watanzania
wenzetu kwa ushirikiano wenu katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa ndugu yetu
Albert Mangweha kilichotokea Afrika Kusini.
-
Katika kufanikisha msiba na mazishi ya ndugu
yetu mpendwa tunapenda kuchukua nafasi hii kukaribisha wizara husika,
mashirika, makampuni na watu binafsi kutoa michango yenu kupitia mitandao ya
simu zifuatazo :
-
Kwa watumiaji wa mtandao Tigo, Nenda kwenye
kutoa pesa toa kiasi unachotaka kuchangia
, kisha andika namba ya wakala 00001 ,ambapo litatokea jina la Mangwair
Contribution hapo utakuwa tayari
umechangia.
-Tigo: Namna ya kuchangia, Nenda
kwenye kutoa pesa , andika namba ya wakala ambayo ni 00001, chagua kiasi
unachotaka kuchangia, Jina litakalokuja
ni Mangwair Contribution baada ya hapo utakuwa umechangia.
-
Mpesa – 0754-967738
Pia kwa kutumia akaunti ya benki ifuatayo:
-
Jina la Akaunti : Kenneth B. Mangweha
Nambari ya Akaunti: 2012505840
Benki : NMB
Pia kwa niaba ya kamati tunapenda kutoa ratiba kama
ifuatavyo:
Mwili wa Ndugu yetu
Albert Mangwea utafika siku ya jumapili ya tarehe 2/06/2013 saa nane mchana na
sio siku ya jumamosi kama ilivyotaarifiwa hapo awali ,
Siku Jumatatu ya
tarehe 03/06/2013 kuanzia saa mbili
asubui mpaka saa sita mchana , ambapo
baada ya hapo safari rasmi ya kuelekea
Morogoro kwa ajili ya mazishi itaanza.
Tukiamini kila mwenye uwezo atachangia katika kufanikisha
shughuli hii tunatanguliza shukurani zetu za dhati.
Pia tunaomba watanzania mujitokeze kwa wingi katika kuaga
mwili wa marehemu katika kuonyesha upendo wetu kwa ndugu yetu Albert Mangweha.
No comments:
Post a Comment