22.11.13

Monday, June 17, 2013

(Photo) Redds Miss Mwanza 2013/14 ni Lucy Charles

Kinyanganyiro cha kumtafuta mnyange wa mkoa wa Mwanza kwa mwaka 2013, kiliteguliwa usiku wa ijumaa baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 13 waliojitokeza.
Nyota ya mrembo huyo ilianza kuonekana mapema, katika mavazi yote aliyovaa, lakini zaidi aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Yatch club baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Judith Josephat na mshindi wa tatu ni Suzan Ikombe.
Washindi hao watawakilisha mkoa wa mwanza katika shindano la kanda mwishoni mwa mwezi huu.

No comments: