MKUU wa
Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Ahmed
Kipozi ameitaka jamii kuakikisha inashughulikia suala la kuwalinda watoto ikiwemo
suala la ukatili, mila kandamizi na utumikishaji husio faa.
Kipozi
alisema hayo jana jumapili alipokuwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku
ya Mtoto wa Afrika inayofanyika kila mwaka Juni 16.
Akihutubia wananchi,
pamoja na watoto wakiwemo kutoka shule mbalimbali
za msingi za Wilaya hiyo, alisema kuwa Jamii inajukumu kubwa ya kuakikisha sula
la ulinzi linatekelezwa kwa pamoja hasa katika kumlinda motto.
“Kumlinda mtoto
na mila kandamizi ni jukumu letu, nasi hatuna budi kuwaakikishia hilo pamoja na
kutokeza vitendo viovu dhidi yao” alisema Kipozi.
Pia alieleza
kuwa wajibu wa kila mmoja ni kuakikisha watoto wanakuwa kwenye ustawi bora
katika makuzi yao ilikuweza kutimiza malengo yao mbalimbali pindi watakapofika
ukubwani.
kwa upande
wake, mmoja wa wazee wa Mila wilayani hapa, Rashid Yusufu Sekamba alisema kuwa watahakikisha wanaachana
na mila potofu ilikuendana na wakati ikiwemo suala la unyago kwa watoto wa
kike.
“Tumesikia
sana kilio chenu watoto, juu ya mila potofu hasa unyago, tutachukua hatua na
hata kulimaliza..
.Mimi sijui
huko kwenye unyago wanafundisha mambo gani, ila kama unamcheza mtoto bado yupo
shule, ni lazima aende akajaribu kwa vitendo hili si sawa. Sasa unadhani hili
ni sawa?, si sawa wazee wa mila tutaangalia namna ya kuachana nalo” alisema
Sekamba.
Katika
maadhimisho hayo, ambayo yaliratibiwa na Halimashahuri ya Bagamoyo kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali, Mkuu wa Wilaya alikabidhi baiskeli moja ya
walemavu (wheelchair), pamoja na kupokea kandambili pea 300, vyote vilivyoolewa
na Asasi ya TRACED.
Sherehe za
mwaka huu za mtoto wa afrika yenye kauli mbiu, “Kuondoa mila potofu zenye
kuleta madhara kwa watoto: Ni jukumu letu sote”.
Kwa upande
wao wajumbe mbalimbali waliotoka asasi za kiraia ndani ya wilaya hiyo
walipongeza shughuli hiyo.
Asasi hizo
ni pamoja na HELP Foundation, Mkombozi, TRACED, HakiMtoto Foundation, BAKA, Compassion
na wengine wengi.
Kwa upande
wa watoto hao waliweza kuelezea na kutoa kero mbalimbali dhidi ya vitendo
wanavyofanyiwa na jamii ikiwemo unyanyasaji na ukatili huku wakiomba kutambua watoto
ni taifa la leo hivyo linahitaji
kulindwa.
Kupitia risala
yao, watoto hao mbele ya DC, walitaka kuthaminiwa,ulinzi, kusikilizwa na yale
yote ya msingi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment