22.11.13

Wednesday, June 12, 2013

(Photo) REDDS MISS MWANZA 2013/14 NI TAMBO NA MAJIGAMBO!!

Washiriki wanaowania taji la Redds Miss Mwanza 2013, wameanza tambo na majigambo ya kunyakua Taji hilo, huku kila mmoja akieleza sifa za kushinda taji hilo. 

Wakiongea kwa nyakati Tofauti wanyange hao walioweka kambi katika Hotel ya New Mwanza, wamesema mwaka huu pamoja na uwepo wa ushindani katika baadhi ya mikoa hapa nchini, lakini mkoa wa Mwanza umeonekana kuwa na warembo wenye ushindani zaidi kufuatia kila mrembo kuwa na vigezo vinavyo stahili, kupelekea kushindwa kutabili nani atabeba taji la Redds Miss Mwanza 2013.Baadhi ya warembo wamefunguka zaidi na kusema, mikoa ya kanda ya ziwa inayoleta warembo wao katika Kanda mkoani Mwanza, wajipange zaidi kwani Mwaka huu, Taji la kanda litabaki Mwanza na hata taji la Miss Tanzania litarejea Mwanza, kwani historia inaonyesha mkoa wa Mwanza ndio wenye Historia ya kuchukua Taji la Miss Tanzania mara mbili Mfululizo, ambapo Mwaka 2008 alilichukua Nasreem Karim na mwaka 2009 Miriam Gerald akalichukua tena.Jumla ya warembo 14 watapanda jukwaani katika ukumbi wa Yatch Club Mwanza siku ya Ijumaa ya terehe 14/06/2013 kuanzia saa 2 usiku.Warembo hao ni pamoja na Catherine Steven (21), Rose Peter (22), Victoria Newton (22), Clara Henry (20), Everlyn Charles (22), Esta Perfect (19), Edna Celestine (18), Judith Josephat (20), Lucy Charles (23), Nasra Muna (20), Suzan Ikombe (20), Khadija Suddy (20), Angel Lawrence (22), na Hajra Mohammed (22).

Mpambano huu utasindikizwa na Burudani la kufa mtu toka kwa CHEGE na SNURA. 

No comments: