22.11.13

Friday, July 26, 2013

(News) MKAZI WA IRINGA ACHUKUA KITITA CHAKE KUPITIA PROMOSHENI YA CHEKA PLUS YA VODACOM.

 Meneja wa Vodashop  Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro(kulia)akimuelekeza jinsi ya kutoa Pesa,Anatori E.Chogolo-mkazi wa Iringa,(katikati)ambae ni mshindi kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja katika Promosheni ya Cheka Plus,alizotumiwa kwa njia ya M-PESA  kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)na Meneja wa Vodashop  Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro(katikati)wakimshuhudia Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Plus Bw.Anatori E.Chogolo-mkazi wa Iringa,ambae ni mshindi ,kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu,akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Pesa alizokabidhiwa mara baada ya kuzitoa kwa njia ya M-PESA,alizotumiwa kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo,ili kujiunga na promosheni hiyo wateja wanatakiwa kupiga *149*01#

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akimkabidhi Tsh milioni 2  Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Plus Bw. Anatori Emmanuel Chogolo-mkazi wa Iringa,ambae ni mshindi ,kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,baada ya kuzitoa kwenye M PESA alizotumiwa toka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu.Ili kujiunga na promosheni hiyo piga *149*01#

Mmoja wa washindi wa droo kubwa kati ya washindi 5 wa Promosheni ya Cheka Plus Bw. Anatori E. Chogolo-mkazi wa Iringa(katikati)akihesabu Pesa zake Shilingi Milioni 2 mara baada ya kuzitoa kwa njia ya M-PESA,alizotumiwa kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo,wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom,Matina Nkurlu na kulia ni Meneja wa Vodashop Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro.

No comments: