22.11.13

Thursday, July 25, 2013

(News) R.O.M.A: WAKATI MWINGINE NATAMANI SANA NAMIMI NIIMBE MAMBO MENGINE KAMA WENZANGU!!! KAMA WASANII WENGINE!!

NATAMANI SANA NAMIMI NITOE NYIMBO VERSES ZOTE TATU NAJISIFIA TU KUWA :-
MIMI MKALI WA UANDISHI/
MIMI MKALI WA STAGE/
MIMI MKALI WA HIP HOP!!

NATAMANI SANA KUMUIMBIA HATA MPENZI WANGU AU KUWASILISHA HISIA ZA MAPENZI KTK NYIMBO MAANA HATA MIMI NI BINADAMU!! NA NINA HISIA!!

AISEE NATAMANI SANA KUIMBIA BATA/ MAANA NATOKAGA VIWANJA SANA NA NATAMANI NAMI NITOE HATA NGOMA YA KUHAMASISHA WATU KULA BATA!!
IITWE HATA NJOONI TURUKE KWANJA(hahahahahha eti roma atoa ngoma mpya yaitwa NJOONI TURUKE KWANJA)!! sijui kama mtasikiliza radio!!lol

NATAMANI KUIMBA KUHUSU VITU VINGI SANA KAMA WASANII WENGINE!!!

LAKINI SASAAAAA

NAJIONA NINA MZIGO MKUBWA SANA NA NIMEBEBA MABEHEWA YA WATU WEEENGII SAANA WANAOTAKA NIWAWAKILISHIE SHIDA NA DHIKI ZAO KUPITIA MZIKI HUU!!

WATU WANGU WA GEITA NA MIGODI MINGINE KILA SIKU WANANIAMBIA WANATESEKA KULE MGODINI HAWAPATI HAKI ZAO!!
SO NI MIMI WAMENITUMA NIWAWAKILISHIE KERO ZAO NA WANANIITIKIA!!

WALE WATU WANGU WA MTWARA WANATAKA SANA KUSIKIA NENO LA ROMA KUHUSU SAKATA LAO LILE LA GESI!!
KUWA ITOLEWE BASI HATA ELIMU BORA JUU YA RASILIMALI ZAO NA ZA WATANZANIA KIUJUMLA!! ILI MACHAFUKO YASITOKEE NA AMANI ITAWALE!!
(wale waliokufa ni mashabiki wetu na wangu naamini hivo)!!

NINA WATOTO WA MTAANI WENGI SANA WANALALAMIKA HATA NITOE KIBAO KWA AJILI YA KUWAFARIJI!!

WAPO WAGONJWA AMBAO WAKISIKIA SAUTI YANGU WANAPATA AHUENI NA HASA WANATAKA NIENDELEE KUIMBA VINAVYOWAGUSA!!(napitaga mahospitalini sana na nayaona haya)!!

WALALAHOI WENZANGU WANANIONA MIMI KAMA BALOZI WAO NIWAWAKILISHE KWA TUNGO ZA HAKI NA UKWELI!!

WANAFUNZI WA MADARASA NA LEVO MBALI MBALI HUFARIJIKA NIKIWAKILISHA ZILE DUKUDUKU ZAO!!

NA PIA KUSHAURI NINI KIFANYIKE NA INASAIDIA SANA!!
FROM TANZANIA HADI 2030!!! (though bado mengi kutekelezwa!!)

Sasa kuna wakati najiuliza kwanini niiimbie POMBE?? wakati kuna bibi yangu kule bush mazao yake hayasogei?
ingawaje nayeye siku yakisogea ataisogelea POMBE hiyo hiyo!!( hahahahahahahh MAISHA BANA)!!

- NAPENDA NITOE NYIMBO AMBAYO UKIISIKIA ITAKUHAMASISHA
KUMRUDIA MUNGU WAKO- adhana ikiliaaaa.....

-PIA ITAKUHAMASISHA KUJIPANGA WEWE NA FAMILIA YAKO KWA MAISHA YA KESHO- mzee wa bandari kastaafu kajenga banda la uani ana wake watatu....

- ILA PIA ITAKUHAMASISHA UFANYE KAZI KWA BIDII...utajiri upo kaburini/ marehemu hufa na chake pigana upate chako!!

SIO MBAYA KWA WANOFANYA...ila SIPENDI KUFANYA NYIMBO ITAKAYO KUHAMASISHA WEWE YANI UKIISIKIA TU UWAZE NGONO/ MAPENZI/ANASA NA VITU KAMA HIZO!!

SIO MBAYA NA KWA WANAOFANYA WANAITENDEA HAKI SANAA!!
MAANA SANAA INA WIGO MPANA SANA!!

ILA KWA SASA ROMA HAJAAMUA KUIFANYA SANAA KTK NJIA HIYO...ITAKAPOBIDI BASI TUTAFANYA!!!(wengi huuliza kuhusu nyonga washa vuta rais wa getho!!)

"SIKILIZA NYIMBO AMBAYO ITAKUFANYA UAMKE NA KUINGIA UVUNGUNI MWA KITANDA NA KUBEBA JEMBE KWENDA PIGA KAZI,
HUKU UKIELEKEA SHAMBA UNA KAREDIO KAKO KAMKULIMA UNASIKILIZA NYIMBO HIYO NA INA KU-INSPIRE"!!!

NIOMBEENI UZIMA MARAFIKI
Round hii nita deal na wao PERPENDICULAR!!

Says Rooomaaaaa!!!!!!!

7 comments:

makota hassan said...

genius

GODFREY KISAVA said...

nice joh!#roma

Dogo Mjanja said...

safi sana, hiyo ndo Hip hop halisi. keep it up

Anonymous said...

Romaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.....Always unawazaga postive Ninja

Anonymous said...

jana nilikuwa kwenye daladala kikagongwa kitu cha mathematics... Dah nikakisikiliza ila kiu haikuisha nimefika geto tu nikafungua folder la ROMA na kusikiza ngoma zote... Ebana ee makitu ya huyu jamaa sio mchezo ni darasa tosha yaan ni hip pop kweli. Wajifunze wengine kuna mambo kibao ya msingi wanaharakati wa hip pop mnabidi myachikonoe... Fanyeni hivyo basi

Anonymous said...

nc dude.........

Anonymous said...

Hvy ndvyo fwexy