22.11.13

Monday, July 29, 2013

(Photo's) Msanii DAYNA atembelea kaburi la ALBERT MANGWEHA huko Morogoro

  Msanii wa bongo fleva Dayna Nyange anayewakilisha mkoa wa Morogoro pichani akiweka Mshumaa juu ya Kaburi la Mangweha.

Dayna amesema Albert Mangweha ni moja ya wasanii aliokuwa nao karibu sana na alikuwa  akimsaidia kwa mambo mengi sana katika mziki
   "Unajua Albert Mangwea ni zaidi ya msanii mwenzangu, alikuwa kama ndugu kwangu. Albart alikuwa akinishauri mambo mengi sana juu ya mziki na hata maisha pia. Hivyo ni wajibu kwangu kumkumbuka mara kwa mara. Pia kitu ambacho hukijui, Ngwea ni moja ya wasanii walionisaidia sana hasa kusambaza wimbo wangu huu wa sasa nilioimba na Mr: Blue - Leo. sitamsahau my Brother Ngwea  na ndiyo maana ndani ya mwezi mtukufu nimetenga siku ya leo kuja kumtembelea. Pumzika kwa amani japo pengo lako bado lipo'' Amemaliza huku akibubujikwa na machozi.
 Dayna akipiga saluti ishara ya kumkubali Marehemu Albert Mangweha
Pumzika kwa amani Ngwea.

3 comments:

Anonymous said...

safi mdada

Anonymous said...

big up

Abubakar kivumbi said...

BIG UP DADA