22.11.13

Sunday, August 18, 2013

(News) #DJCHOKAblogTOP10 August 18,2013

Hii ndio chat yetu ilivyokuwa kwa week hii inayoisha, mabadiliko ni mengi sana kama wewe ni mfuatiliaji wa chat hii utajionea mwenyewe jinsi nyimbo zinavyopanda na kushuka. Rama Dee na wimbo wake wa KAMA HUWEZI bado unaendelea kukimbiza namba moja kwa wiki ya 4 sasa.

AY na Mwana FA wimbo wao wa BILA KUKUNJA GOTI kutoka nafasi ya 5 kwa wiki 3 mfululizo safari hii umekuwa namba 8. Wimbo wa Lady JayDee YAHAYA kutoka namba 3 wiki iliyopita leo tunaona amekuwa namba 5. Wimbo mpya wa Ommy Dimpoz kutoka namba 10 hadi namba 3 pia unakimbizana na wimbo wa Nay wa Mitego ambao uliingia pamoja kutoka namba 9 mpaka namba 4 wiki hii. Nyimbo mbili zinazotoka wiki hii ni wimbo wa Baghdad pamoja na wimbo wa Snura ambazo zilipata kura chache sana. Je unahisi wiki ya kesho ni nyimbo gani mbili zitaingia kwenye chat na kusumbua wenzake kama hizi zilizoingia wiki iliyopita na kufika top 5 ya juu?

Stay tune...for more info chat with me by SMS DJCHOKA SEND TO 15678

1 comment:

bryan majenga said...

Chibwa ft Juru Nishai bonge ya Ngoma