22.11.13

Friday, September 06, 2013

(News) Shule ya Msingi Lukugu iliyopo Wilaya ya Missungwi -Mwanza yakabidhiwa vifaa vya michezo

 MenejaUhusiano wa Njewa Vodacom Salum Mwalim akiongea kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Vodacom kwa shule ya Msingi Lukugu iliyopo Wilaya ya Missungwi mkani Mwanza. Kushoto kwake ni Meneja wa Vodacom Missungwi Gift Tesha na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Kishiwa Maleba (wapilikushoto).

 Meneja wa Vodacom Wilaya ya Missungwi Gift Tesha akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lukungu jezi zilizotolewa na Vodacom.Kampuni hiyo  imeipatia shule hiyo jezi za mpira wa pete na soka pamoja na mipira ili kuendeleza michezo shuleni hapo ya kukuza michezo nchini. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

 Meneja Uhusiano wa Njewa Vodacom Salum Mwalim akimkabidhi Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Msingi Lukungu iliyopo Wilaya ya Missungwi Vicent Ndulu moja ya mipira iliyotolewa na Vodacom pamoja na jezi kuendeleza michezo shuleni hapo.  Katikati ni Menejawa Vodacom Missungwi Gift Tesha.

 Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha Star TV Abdala Tilata akishauriana jambo na Meneja wa Vodacom wilaya ya Missungwi Gift Tesha(katikati) na MenejaUhusiano wa Nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim muda mfupi kabla ya Vodacom kukabidhi vifaa vya michezo kwa shule ya MsingiLukungu iliyopo Wilayani Missungiwi Mkoani Mwanza. 

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lukungu iliyopo Wilaya ya Missungi  Mkoani Mwanza wakifurahia kupokea vifaa vya michezo kutoka kampuni yaVodacom walivyokabidhiwa ilikushiriki vema katika shughuli za michezo wawepo shuleni. Vifaa vilivyotolewa ni jezi seti mbili za mpira wa soka, seti moja ya mpira wa pete, mipira na fulana za mazoezi.

No comments: