Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akishirikiana na Mkuu wa Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa kukagua vifaa vya michezo muda mfupi kabla
ya Waziri kukabidhiwa rasmi vifaa hivyo vitakavyotumika kwenye mashindano
maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa
Vodacom Salum Mwalim.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea vifaa vya michezo kutoka
kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa. Vifaa hivyo
vitatumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto
ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom ilikabidhi jezi za
soka seti 12, mipira 40 na kombe kubwa la Mshindi
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea kombe kubwa kutoka kwa Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa atakalokabidhiwa mshindi wa
kwanza wa mashindano maalum kwa shule za sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa
na Wizara.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Yasoda. Vodacom ilikabidhi
pia jezi za soka seti 12 na mipira 40.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangala akiongea na waandishi wa habari
wakati wa hafla ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo vilivyotolewa na
Vodacom kwa ajili ya mashindano maalum kwa shule za sekondari za mkoa wa Dar es
salaam yanayoandaliwa na Wizara.
Waandishi wa Habari wakimfuatilia
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangala wakati
akiongea kwenye hafla ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo kutoka Vodacom
vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya shule za Sekondari Mkoa wa Dar es
salaam yanayoandaliwa na Wizara.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
Vodacom Kelvin Twissa akifanunua jambo kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Dk. Fenela Mukangala wakati walipofanya mazungumzo mafupi baada ya
hafla ya amkabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano maalum ya
shule za Sekondari za Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje
wa Vodacom Salum Mwalim.
No comments:
Post a Comment