22.11.13

Sunday, September 08, 2013

(Photo's) Yaliyojiri kwenye show ya Kilimanjaro Music Tour 2013 KAHAMA

 Kwa mara ya kwanza katika historia ya mji wa Kahama na vitongoji vyake, wakazi wake walipata nafasi ya kuwashuhudia wakali wa muziki zaidi ya 10 katika jukwaa moja katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 lililofanyika katika uwanja wa taiga Kahama na kushuhudiwa na maelfu ya wakazi wa rika zote waliojitokeza na kuujaza uwanja wote.  Wakali hao Linex, Profesa Jay, Roma, Ben Pol, Fid. Q, Lady Jaydee, Izzo Bizness, Barnaba na Recho walilishambulia jukwaa kwa masaa sita mfululizo huku wakati mmoja wakipata nafasi ya kumuimbia Ben Pol wimbo wa Birthday kutokana na kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa usiku wa kuamkia Jumapili.

 Linex

 Shabiki mmoja alipata nafasi ya kucheza na Recho

 Kutoka backstage: Izzo Bizness, Alice, Fid Q, Kala Jeremiah na Ben Pol

 Ben Pol na Alice wakiimba wimbo wao mpya wa Waubani

 Barnaba Boy jukwaani

 Izzo Bishara, Izzo Bizness akiiwakilisha Mbeya mjini Kahama

 Izzo Bizness na Barnaba wakishambulia jukwaa kwa pamoja

 Baada ya kushuka jukwaani mashabiki hawakutaka kupoteza nafasi ya kupiga nae picha.

 Kala Jeremiah akiwauliza mashabiki kama wameilewa Kikwetu kwetu

 Jibu la mashabiki lilikuwa ni hili

 Roma Mkatoliki akiwarusha mashabiki waliofurika uwanja wa taifa Kahama

 Lady Jaydee na Profesa Jay wakiimba Joto Hasira

 Profesa Jay akiifunga Kili Music Tour Kahama

Mashabiki wakinyoosha mikono juu kuwashukuru wakali wa muziki waliopanda jukwaani