22.11.13

Wednesday, October 23, 2013

(News) JANJARO: SIJAFUKUZWA NA OSTAZ JUMA ILA NIMEJITOA MWENYEWE MTANASHATI

 Janjaro msanii kutoka Arusha lakini makazi yake yapo Dar amefunguka na DJCHOKAblog kuwa hajafukuza na Ostaz Juma Namusoma kwenye kampuni yake ya Mtanashati bali amejitoa mwenyewe kwa hiari yake. Janjaro amesema amechoka na matendo tu ya Ostaz na alikuwa tu akiyavumilia lakini kwa sasa ameshakuwa mkubwa so nataka nikae kivyangu vyangu nifanye mambo yangu kama wasanii wengine ambao hawana meneja na wanafanya poa. Namnukuu Janjaro akisema....
 "Najua yatasemwa mengi kutoka kwa Ostaz Juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna watu wanasema sina utovu wa nidhamu lakini hao watakuwa wananijua sasa hivi hawajanifuatilia kutoka nyuma. Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa mkubwa hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa pelekwa tena sitaki, kwa maelezo zaidi Ostaz Juma aongee na wazazi wangu asiongee na mimi"


No comments: