22.11.13

Monday, October 21, 2013

(News) Rais Kikwete Azindua Mnara wa Vodacom Njombe

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Meneja wa Vodacom wilaya ya Makambako Benedict Kitogwa  wakati Rais Kikwete alipofika kuzindua mnara wa 3G wa kampuni ya Vodacom ikiwa ni moja kati ya minara mipya 16 ambayo kampuni hiyo inaijenga Njombe kwa lengo la kuboresha huduma na kuwawezesha wakazi wa Njombe kuwa na huduma za uhakika za intaneti. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uhandisi wa Vodacom Nguvu Kamando na Kulia ni Meneja wa kampuni hiyo Wilaya ya Njombe Leonard Kameta.

 Rais Jakaya Kikwete akiuzindua rasmi mnara wa Vodacom wa 3G Mjini Njombe utakaowawezesha wakaiz wa mji huo na vitongoji vyake kuweza kupata huduma za Intaneti kupitia simu zao za mkononi. Vodacom inajenga minara mipya 16 kwa lengo la kuboresha huduma zake na kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi. 

Rais Jakaya Kikwete akisoma kibao cha jiwe la uzinduzi wa manta wa 35 wa kampuni ya Vodacom mara baada ya kuuzindua mjini Njombe mwishoni mwa wiki.  Vodacom inajenga minara mipya 16 kwa lengo la kuboresha huduma zake na kuwawezesha wananchi kuwa na uhakika wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi mkoani humo.

No comments: