22.11.13

Sunday, November 17, 2013

(News) Vodacom yazidi kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma zake

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bw. Yusuph Mwenda(katikati) akisikiliza jambo toka kwa Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh(kulia) muda mfupi kabla ya kuzindua  rasmi duka jipya la Vodacom lililopo Shamo Tower Mbezi beach  gorofa ya kwanza jana jijini Dar es Salaam.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Bw. Yusuph Mwenda akikata utepe  ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa duka la Vodacom Tanzania lililopo Shamo Tower Mbezi beach gorofa ya kwanza jijini Dar es Salaam,wengine kulia ni Meneja wa duka hilo,Bw.Kartic Subramaniam na kulia ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Hassan Saleh.

Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Bi.Pendo Richard (kulia) akimuelezea Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda matumizi ya baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika duka jipya la kampuni hiyo,Mara baada ya Meya huyo kuzindua duka hilo jana Shamo Towers gorofa ya kwanza, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo,Bw. Hassan Saleh.

·        Upatikanaji wa huduma za Vodacom wazidi kurahisishwa
Dar Es Salaam 17 Novemba 2013… Katika kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wateja wake na kuwaridhisha kwa kile wanachokihitaji, Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza Tanzania Vodacom imezindua duka jipya ambalo litawawezesha wateja mbalimbali wa kampuni hiyo wakiwemo wakazi wa Mbezi Beach kunufaika na upatikanaji wa karibu wa huduma mbalimbali za muhimu za mawasiliano.
Mgeni rasmi katika ufunguzi huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amewaasa wakazi wote wa Mbezi kutumia ipasavyo duka hilo ili kuweza kutatua matatizo yao ya huduma za kimawasiliano.
”Najua walio wengi walikua wakisubiria na kutamani kuona ni muda gani Vodacom itawaletea duka ambalo litawapa huduma mbali mbali za kimawasiliano, sasa kuanzia leo duka limefunguliwa rasmi hivyo mnapaswa kulitumia ipasavyo kwani limewekwa hapa kwaajili yenu wote wateja wa Vodacom”. Alisema
Mwenda aliongeza kuwa “Idadi kubwa ya watanzania ambao ni watumiaji wa huduma za kimawasiliano imekuwa ikiongezeka siku hadi siku, hivyo kufuatia uzinduzi huo itakuwa ni suluhu tosha ya kuwawezesha wateja walioko Mbezi Beach na hata nje kuweza kutatua haja zao pale wanapokuwa wanahitaji huduma”.
Kwa upande wake Ofisa mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Hassan Saleh amesema kampuni yake inatambua mchango unaoendelea kutolewa na wateja wake, hivyo inazidi kuwaunga mkono kwa kuwapa urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa kuwafungulia duka ambalo litawawezesha wakazi wa Mbezi kutokupoteza muda wao mkubwa kwenda mbali kwaajili ya huduma mbalimbali za Vodacom, badala yake kutatua matatizo yao  hapo hapo Mbezi Beach katika duka hilo.
“Mahitaji ya huduma kwa  wateja sasa ni makubwa na watanzania wanahitaji kupata kile watakachokifurahia katika maisha yao ya kila siku. Hivyo Vodacom kupitia duka hilo itawawezesha wakazi wa Mbezi na maeneo mengine kuwa karibu na upatikanaji wa huduma na kuacha kwenda mbali kama walivyokuwa wakifanya apo awali” Alisema Saleh
Akiongezea kuwa “Bado tutaendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma zetu kwa kuzidi kufungua maduka mengi zaidi sehemu mbalimbali ambazo hazijafikiwa na kuhakikisha wateja wetu wote wanaendelea kufurahia huduma zetu za Vodacom, hatimaye kuendelea kubaki kinara kwa kuwapa huduma bora wateja wetu”
Hadi sasa Vodacom inamiliki maduka 72 yaliyo katika sehemu mbalimbali za nchi ambayo yanaendelea kutoa huduma bora na zinazostahili kwa wateja wake kitendo ambacho kinawafanya kuwa ni kampuni inayoongoza hapa nchini.
Upanuzi huu wa wigo wa huduma za mawasiliano ya simu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania unafuatia uwekezaji kwenye mfumo wa mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unaotumia teknolojia mpya ya mawasiliano kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.
Mwisho…

No comments: