Dar es
Salaam, Novemba 2, 2013 … Wafanyakazi
wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania wamefanikiwa kunyakua tuzo za
utendaji bora za kila Mwaka zinazotolewa na umoja wa makampuni hayo Afrika.
Tuzo hizo ambazo hutolewa kila mwaka kwa watu binafsi na
kundi lenye utendaji uliotukuka zimemshuhudia Lilian Mwasha, Mkuu wa Huduma Endelevu,
akijinyakulia tuzo ya kujitolea kwa jamii huku Mkuu wa kitengo cha Uendelezaji
Biashara, M – pesa, Isack Nchunda akijishindia
tuzo ya utendaji binafsi huku tuzo ya timu bora ikienda kwa kitengo cha mauzo
cha kampuni hiyo.
Kwa upande wake Ofisa Mkuu Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali
watu, Fred Mwita, amesema wafanyakazi wa kampuni hiyo wameendelea kujitolea kwa
nguvu zao zote na ndio maana Vodacom imeendelea kuongoza katika soko miaka
yote.
“Kila mwaka
wafanyakazi wa makampuni ya Vodacom kutoka nchi mbalimbali ambazo Vodacom inatoa huduma zake ikijumuisha
nchi za, Tanzania, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo, Afrika ya Kusini
na Lesotho, huchaguliwa na kuhudhulia tuzo hizo ambazo hutolewa Johannesburg
Afrika ya Kusini.
“Washindi wa Tuzo
hizi huchaguliwa kutokana na utendaji wao wenye tija uliozidi viwango vyao vya
majukumu yao ya kila siku, huku tuzo hizo zikiwa sehemu ya kutambua mchango wa
wafanyakazi hao na kuwahamasisha wengine.
“Tunao wafanyakazi
ambao wanachaguliwa katika vipengele mbalimbali vya tuzo zinazotolewa na
kampuni yetu kuanzia kwa mtu mmoja mmoja na wale wanaojitolea katika kazi na
timu bora ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kampuni zetu,
huku tuzo ya ubunifu ikitolewa kwa kwa mtu ambae amekuwa na ubunifu mzuri
katika utendaji wake wa kila siku alisema Meza.
Meza alihitimisha kwa kusema ni jukumu la kila mfanyakazi
wa kampuni hiyo kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii na kwa moyo wake wote ili
kuhakikisa kampuni inafanikiwa na kuendelea kuongeza katika soko na kampuni pia
haitoacha kutambua michango ya wafanyakazi wake kama ilivyofanyika sasa.
Mwisho
. . . .
No comments:
Post a Comment