22.11.13

Tuesday, October 13, 2009

SAFARI YETU YA KWENDA MWANZA ALIKUWA POA SANA.

Huyu ndie dereva wa safari zote za Fiesta One Love, anaitwa Bw. Juma. Jamaa anadrive poa sana wala hana speed zakipumbavu ndio maana tunampenda.

Braza akifikiria safari ya kufika Mwanza itakuwaje maana ni mbali bwana.

Tukiwa safarini lazima tusali, hapa Adam anatusomea mistari iliyoandikwa kwenye Biblia takatifu.

Mr. Blue akiwasiliana na Boss wake Tippo.

Tulipofika Manyoni Singida tukapumzika na Camera za Clouds TV zikaanza kuning'arisha.

Huyu babu hata sijui kwanini alitusimamisha maana alikuwa anaongea ki Singida Singida sasa sijui alikuwa anataka nini, mimi sikumwelewa.

Vumbi la Manyoni jamani usilipimie, wakati tunaanza safari tuliambiwa barabara imetengenezwa lakini ni Wizi mtupu bado kuko vile vile ndugu zangu.

Tukaingia Mwanza salama majira ya saa 12 jioni...hapa ni kituo cha mabasi Nyegezi.

No comments: