22.11.13

Monday, October 12, 2009

SHANGWE ZA FIESTA ONE LOVE JIJINI MWANZA.

Farid Kubanda akiwa nyumbani Mwanza na begani akapewa mkanda kudhihirisha yeye ndio mfalme wa Mwanza kwenye Fiesta One Love.

Mama yangu nimekosea kulitaja jina pale juu, Adam akiwa na B12 wakiwa chini baada ya kuwaita Samaki Samaki wazee wa mduara.

Samaki samaki wakiwa wanapanda jukwaani.

Walikuwa wasanii wa kwanza kupanda jukwaani na kukimbiza vilivyo.

Sasa hili nyomi lilikuwa hivi, huu ni upande wa kulia kwangu.

Hapa ni katikati yangu.

Huku ni kushoto kwangu, daaah wakazi wa mwanza SAFI..

Jose Mtambo mtoto wakigambonino akafuatia.

Wasanii wakiwa kwenye basi kama backstage yao maana wakitoka nje tu balaa wananchi wanafurika wakitaka picha

Izzo Biznes akafuatia na akawakilisha ipasavyo.

Mwanadafada kutoka Bongo Star Search Baby Madaha ikafika zamu yake na mambo yalikuwa bam bam full mtetemesho.

Adam, Maunda na B12 wakishangaa mauno ya Baby Madaha, Unabishaaaaa.

Juxs msanii anayekuja vizuri tu kwenye ulimwengu huu wa music wa kizazi kipya.

Cyrill msanii anayesifika kwa kuvaa GUCCI mpaka kawaambukiza wakina naniliiii.

Ikafikia zamu ya Suma Lee kulitawala jukwaa, hapa akiwa na msanii mwenzake Quick Racka wakiimba wimbo wa Yollanda.

Huyu ndie msanii aliyefunika vibaya katika tamasha la Fiesta One Love Mwanza.

MC Adam Mchomvu akiwa stejini na tayari kumwita Madee.

Huyu jamaa bwana, akiwa stejini anakimbiza vibaya sana, sasa ukifikia wimbo wa Pesa hapo ndipo utamjua Madee ndio nani maana anagawa hela kwa mashabiki wake..

Joh Makini aliwakilisha Hip Hop kuanzia muonekano wake mpaka analivyokuwa anaimba jukwaani..ilikuwa safi sana pale alipopanda na mdogo wake Niki wa pili.

Mtoto kutoka Morogoro mji kasoro bahari Belle 9 alipata shangwe nyingi sana.

Maunda Zorro akiwa kwenye jukwaa la Fiesta Mwanza, alifanya vizuri sana.

Marlaw mzee wa Pi Pi

Chidi Beeeeeeeeeeenz kama kawa akipanda kwa steji mfuniko unakuwa ule ule haina kuremba, cheki kwanza alivyojipanga kushoto Chiku katikati yeye halafu nyuma Body G.

Watoto wa kike wakazimia alipoingia Mr. Blue na Dogo Hamidu, usipimeeeeeeeeeeeee

Wananchi walijaa wakasogezwa mbele ili wanyuma waweze kuenea.

Baada ya kutoka Mr. Blue akaingia Cowbama vijana kutoka Zizzou Entertainment, Mangwea kama kawaida yake kaingia na kuanza kuwapa freestyle.

Mfalme wa Mwanza Ngosha ze Don akaingia bwana, full kelele alipopanda na Matonya na kuimba Usinikubali Haraka haraka

Jita Man msanii kutoka Mwanza alipewa respect yake na kupandishwa juu ya jukwaa ili wananchi wamuone maana ilisemekana alikufa baada ya ajali mbaya aliyopata na Piki Piki

Hapa akisaidiwa kushushwa jukwaani na msanii mwenzake Fid Q.

No comments: