Kiukweli nimevumila nimeshindwa, ni hivi kama wewe umefungua Blog au Website na unajua hauna habari zozote zakuweka katika hiyo Blog/Website basi ni bora ufanye shughuli zingine. Sijakataza kuchukua habari ndani ya BONGO STAR LINK na ukaweka kwako lakini mbona husemi umetoa sehemu gani, unachange picha lakini news unagelezea.
Kinachoniuma zaidi unakuta kuna Blog/Website zingine zinawadhamini kabisa na wanakaa tu kazi kuchukua news kutoka sehemu nyingine na kusema katika barua ya udhamini anaoomba kuwa anazitafuta yeye. Wengine ni kutoka magazetini hupenda kuchukua picha na habari hata kusema kwa hisani ya nani yeye anaandika NA MWANDISHI WETU halafu anataja jina lake ndio nini sasa.
Wale wasanii wanatuma mail za nyimbo zao mpya hakikisha wakati unatuma wimbo wako tuma na picha yako ili wadau waweze kukutambua wewe uliyeimba kwa njia ya picha na maelezo ya huo wimbo wako. Nyimbo na picha zenu utazituma kupitia mail yangu ya djchoka@yahoo.com au djchoka@gmail.com na sio mail nyingine mbali na hizo nilizozitaja hapo.
Watu wamatangazo mnayotuma kuanzia tarehe 1 mwezi wa 9 mnatakiwa mkituma TANGAZO la biashara basi inakulazimu kuchangia kidogo ili na sisi huku maisha yaendelee, kwa mawasiliano zaidi mnaweza kutucheki kupitia simu ya mkononi +255 715 727873 au +255 683 164282, au kwa mail ya djchoka@yahoo.com au djchoka@gmail.com
Tucheki kupitia:
Facebook PAGE: Bongo Star Link OR Like DJ CHOKA
Twitter: @BongoStarLink OR @ChokaDJ
Youtube: www.youtube.com/84Choka
E-mail: djchoka@yahoo.com OR djchoka@gmail.com
SORRY KWA USUMBUFU UTAKAOTOKEA.
Per More Jah...
9 comments:
Wachaneeeeeeeee HAO, maana sasa tunatembelea blog mambo ni yale yale tu wakati wengine wanataabika, big up choka
Leo umefunguka ndugu yangu hadi nimeipenda hii...wanachotakiwa kama ulivyosema tu watoe big up tu kwamba picha au habari ni kwahisani ya mtu fulani au blog fulani, mbona wewe unasemaga kwa hisani ya Michuzi na news zinaendelea
safi ujumbe utakuwa umewafikia tu..
kwenye burudani huna mpidhani waache waigilizie tu mwisho watachoka
Kama ipo ipo tu choka kaza buti mdogo wangu...
Aisha KIMARA
INAHUSU...Watajiju bwana wee endeleza bakora
BABA NA WEWE UANDIKE UNAPOTOA
kudadeki naona umefukunga kaka...to me sina neno ni haki yako bana lazima useme unalotaka na hamna haja yakuweka SORRY wala nini ni ujumbe na ufike kwa wahusika na hili lakulipia matangazo ungelirudia kwa herufi kubwa maana ndo mpango mzima sio...Big Up Choka,
Kinega. hapa
mbona na wewe hauandiki unapotoa zako au unakua umeoteshwa?
Post a Comment