22.11.13

Saturday, November 05, 2011

FFU wa Ngoma Africa band wameachia CD "Shangwe 50 Uhuru Annivesary"

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU,yanye
makao yake nchini Ujerumani,wameachia hewani CD mpya yenye nyimbo za miaka 50
ya Uhuru.Nyimbo zilizomo katika CD hiyo ni utunzi na uimbaji wake kiongozi wa bendi
hiyo Kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na Chris-B,mpiga solo wa kikosi
hiko,habari za uhakika zimetonya kuwa nyimbo hizo zimetua pia katika blog mashuuri
ya Michuzi,pia vituo vya Redio vya Deutche Welle mjini Bonn,Radio VOA ya Washington,
Radio Free Africa,Mwanza,vimepoke nyimbo hizo ambazo wakati wowote zinaweza
kutoa burudani kwa wananchi katika shamra shamra za miaka 50 ya uhuru.
Nyimbo hizo mbili     (1) Miaka 50 Uhuru(rumba) na 2. 50 Uhuru Shangwe,
Zinasikia pia at www.ngoma-africa.com

No comments: