22.11.13

Wednesday, May 15, 2013

(News) SABABU ZA MATONYA KUTOSHIRIKI SHOW YA MIAKA 13 YA LADY JAYDEE

Tetesi zinaweza kuwa za ukweli au pengine zikawa ni story za kujitungia
Lakini tetesi zinasema kuwa Matonya alipigiwa simu na wazee wa fitna mara tu waliposkia kluwa atashiriki onyesho la miaka 13 ya JayDee, wakamwambia aachane na hiyo show na kuwa watampa hela ambayo angelipwa kwenye show hiyo.

Na pia wangemuandalia show yake mwenyewe kubwa zaidi ya hiyo miaka 13 ya JayDee
Hizo ni fununu, ambazo hazina uhakika.
Lakini tukirudi upande wa Matonya ambae alishapokea mpaka malipo ya awali na kukubali kufanya show baadae akachomoa ni kama ifuatavyo.

MATONYA: Kaka kumbe tarehe ni lini kumbe:

CAPTAIN:    Ni Ijumaa tar 31 May 2013 kaka mwezi ujao. Tutakuwa na Linah, Jay, Barnaba, Matonya, TID, hamza Kalala

MATONYA: Kaka kumradh sana kuimba na band kwasasa sitoweza manake mtaitaji mandalizi makubwa ili nifanye kazi vzr_ningeomba nitizamwe ktk kazi ingine bro kumradh sana

CAPTAIN: Du! Nshatangaza ilikuwa kaka lakini sawa. Je ntapata ile hela kka nilipe wengine ndg yangu
 
MATONYA: Aisee hata nimekosa raha kukujuza iliswala br_kesho satano mtampa yule rafkiangu anaitwa pizon_walikuja kuleta ile pesa yagari kwaio wataileta apo apo oficen

CAPTAIN: Sawa kaka usijali, Nitashukuru akiileta ili huku nisipate lawama
MATONYA: ok bro

Mara kimyaaaaaaa....... baada ya siku mbili tatu maongezi yakaendelea

CAPTAIN: Naam kaka mzigo haujaletwa. Tafadhali ileteni tu hiyo hela ya watu kaka mi napewa lawama isitoshe we ni ndugu yangu usikubali hela ndogo iharibu.

MATONYA: Gadna aiwezi kuwa ivyo_kuna mapungufu kidgo nayaweka sawa uipate kumradh sana brother

CAPTAIN: Asante

Siku ikapita tena

MATONYA: Kaka kdg kunamisteki nimecheza,, lakini wiki hii haitapita mtakuona bro nimekwama kaka lakini ntajua cha haraka

CAPTAIN: Sijaelewa kaka ni laki **** tu kunirudishia nduguyo nilipe wasanii wengine kwani kuna tatizo au

MATONYA: Bro naskia haya - skutaka hata kuku2mia msg mlitaka ni2we namzigo 2 ila kunambio kdg zimekwamisha nikaona bora kukujuza kuliko kukaa kimya bro tatizo haliwezi

CAPTAIN: Sawa we ni ndugu yangu, basi nisaidie tu irudi hiyo advance niliyokupa ili uniepushe na lawama huku kaka. Au niende kwa bimkubwa Tanga nikalalamike? Ha haaaa haaa

CAPTAIN: Fanya hivyo mdogo wangu nilitaka uwepo ktk show kwa upendo tu lakini haijawa, basi nisaidie tu kurudisha hiyo advance maana nadaiwa na wasanii wengine niwape. Au sio?

MATONYA: Kaka nibendi ndio haya yangu kwasasa nastaki kuharibu kaziyako bora niwe mkweli.. Naswala lako halitoki kichwani bro

CAPTAIN: Sawa jamaa yangu, basi nisaidie ile advance irudi ili niweke mambo sawa huku, mimi sina mdhamini mpaka leo aliyetoa hela, najitegemea tu mfukoni, naomba nirudishie nilipe wengine..Au namoro matonya we ni ndugu yangu?

MATONYA: Sawa brother mtalisimamia soon nikuweke sawa sawa brother - akuna litakalo shindikana kaka amini 2

CAPTAIN: Utarudisha lini nipe uhakika kaka, niko na shida

Adavance ilitoka tangu mwishoni mwa mwezi April
Mazungumzo ndio kama hayo mmeyasoma
Mpaka blog inaingia mitamboni leo, advance haijarudishwa na hakuna jibu la kueleweka.

Wazee wa fitana kama zile tetesi ni kweli kuwa mmemzuia Matonya asifanya hii show ya miaka 13 ya JayDee, na hela ameshaitumia! Kwanini msimsaidie kuirejesha mambo yaishe??

3 comments:

charles said...

dah hao hao ndo wanadai wanakuza muziki,how???!!shame on them na Mungu atawalipa wanachostahili,time heals everythings!

Anonymous said...

Bongo watu wenye senti ni washenzi tu,,, Yaani hawa wasanii wa bongo ni makunguru sana,, badala ya kumsupport mwenzao, wanaweka hela mbele na kuogopa kuwa nyimbo zao hazita pigwa redion. Washenzi wakubwa ndio mana wanashuka kimziki kila siku. Jide komaa nao mbwa hao, wezi, wadhulumati, na mahakama zao za kuficha aibu zao, shenzi kabisa.

Anonymous said...

na wewe gadna m promote Jide nje ya nchi aache kuhemea vi-shoo vya bongo. Muda wake unapita na hujawa meneja mzuri. Wewe ungetakiwa sasa uwe unasafiri na Jide kwenye concert mbali mbali za kimataifa na kumpatia mkataba wa Sony record company. You are part of killing her talent kwa kumuingiza kwenye biashara za migahawa na mapishi mapishi sasa anagombania choo na kina Lina, Barnaba na Matonya!!