Mwanamuziki
kutoka Uganda, Dr. Jose Chameleon anatarajiwa kufanya onyesho kali kesho kwenye
ukumbi mpya wa burudani wa Escape Complex.
Chameleon,
ambaye ndie mwanamuziki mashuhuri kuliko wote kwenye ukanda huu wa Afrrika
Mashariki anatarajiwa kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es Salaam kwa kuimba
nyimbo zake zote kali, ikiwemo Valuvalu.
Usiku huo wa Chameleon utaenda sambamba na burudani kali kutoka kwa MA DJ wakali, DJ Pac na DJ Senorita ambao watafanya show ya utangulizi.
Akizungumzia
burudani hizo, Meneja Uendelezi wa Biashara wa Escape Complex, Anthony David,
alisema watu watarajie burudani kali siku ya jumamosi hasa kwa kuwa sherehe hizo
zitaenda sambamba na sherehe za Eid za pale Escape Complex.
‘Kama
lilivyo jina lake, Escape ni mahali ambapo mtu anakuja kupumzika kukwepa
mihangaiko ya kila siku, iwe kikazi au kimaisha, lakini Eid hii tumeandaa
burudani hii ili kuwapa wakazi wa Dar es Salaam kitu tofauti’ anasema Anthony.
Mbali
na Chameleon siku ya jumamosi, Escape Complex imeandaa burudani siku ya Eid Mosi,
ambapo DJ maarufu Boni Luv atatoa burudani kali, na siku ya Jumpili, bendi
inayokuja kwa kasi Skylight, itawaburudisha wapenzi wake kuanzia asubuhi ili
kuimaliza wikiendi ndefu.
Escape
Complex, ambayo ipo Mikocheni/Kawe karibu nyuma ya ukumbi wa Safari Carnival,
ni Club mpya ambayo inapendezeshwa na ufukwe pamoja na mandhari ya kuvutia,
pamoja na chakula kizuri kwa wateja wake.
Mashabiki
wa Chameleon watalipia shilingi elfu kumi na tano ili kuburudishwa na
mwanamuziki huyo mashuhuri. Na VIP watalipa elfu 40,000/= ikiwemo kinywaji cha
bure pamoja na nafasi ya kumuona msanii huyo baada ya maonyesho.
No comments:
Post a Comment