22.11.13

Tuesday, March 17, 2009

MAISHA PLUS - WASHIRIKI WAWILI WAYAAGA MASHINDANO.

Washiriki wawili waliokuwa wakiwakilisha kanda ya kati, Efrancia Mangii na Peter Putir wameliaga shindano la Maisha Plus hilo huku Maulid Wadi akirejea baada ya kupata kura nyingi.

Washiriki hao wamefungua dimba la kuaga katika shindano hilo lililoanza wiki mbili zilizopita.
Shindano hilo linabakiwa na mshiriki mmoja anayewakilisha kanda hiyo, Juma Madaraka.
Wakati huohuo Putir ameapta shavu la kutangaza katika kituo cha redio cha TBC Fm mara baada ya utolewa katia shindano hilo.
Mkurugenzi wa TBC, Tido Mhando aliitangaza ofa hiyo wa Putir baada ya uvutiwa na sauti nzuri ya mshiriki huyo.

58 comments:

Anonymous said...

Kipindi cha maisha plus kina kasoro kubwa. Baadhi yetu hatuelewi kwanini muda mwingi kamera yenu inamwonyesha Mpemba Abdul.Lengo ni nini hasa? kumpa umaarufu au nini? Hali imekuwa mbaya kiasi ambacho wasichana anaoshindana nao wiki hii kwa lengo la kuwatoa washiriki 2 hawajulikani kabisa. wala mabinti hao hawapewi muda wa kujieleza kama ilivyokuwa kwa wenzao wiki jana!!Kipindi kinahujumiwa.Matokeo yake kura nyingi zinapigwa kishabiki kumchagua Abdul aweze kubaki.AIBU KUBWA.

Anonymous said...

Mshiriki kutoka Tanga ameonesha ukomavu wa akili kweli kweli maana ameweza kudhihirisha kuwa alikuwa mshindani hasa. Hawa wenzake wawili wametia aibu na doa kubwa mashindano haya, hivi kumbe kutolewa na kubaki yote ni vibaya eeh!. Sasa kuzimia kule nini maana yake. Watanzania acheni ushabiki na u-mimi kwenye suala la maisha ya watu. Kura zenu za chuki zinawatoa washindani na kubakisha watafutaji, ndio maana tunaposhindana kimataifa tukishindwa hatukosi visingizio.

Anonymous said...

Hi, mimi naitwa Hadjara na fanyakazi Alliance française ya Dar es Salaam,mimi napenda sana washiriki wa kiume kwani wako juu kuliko wakike wambea mno hasahasa modesta na tedd, mimi mshikiri ninayempa support kubwa ni mshiriki na namba 32 Abdul namfagiliya sanaaaaaaaaaaa kwa upande wa mwingine nampenda upendo na moshi. nawatakiya kila la rheri.

Anonymous said...

jamani tuwewakweli na kura tuzitoe sehemu zinafaa, kwanini asingetolewa mmoja baada ya juma kuacha kuaga mashindano, kwani levina alikua anastahili kubaki kijijini kura yangu mimi ni ABDUL number 32 kutoka pwani acheni chuki binafsi asionekani kwanini na yeye ndiye kiboooooooko yao akitolea maisha plus sitazami tena kwani anaweza sana uyo mshkaji pia charles anapendeza pia kwenye screen mimi ni Sara DSM.

Asha Hussein said...

Hi naitwa A. Hussein, nawapongeza waandaaji wa kipindi cha maisha plus, nampongeza sana mshiriki wa tanga kwa ujasili aliounyesha hakika huyo ni mshindani, jamani huyo mpiga picha kwa nini anamlenga Abdul peke yake? kila kipindi anaonyeshwa Abdul,kwa nini msituonyeshe washikiri wote? Si vizuri tunaomba irekebishwe. Kipindi ni kizuri nakifagilia sanaaaaaa

Anonymous said...

Hi mi nawapa big up sana waandaji wa maisha plus na mshiriki ninae mupenda ki ukweli ni ABDUL namba 32 mana anachangamusha kipindi kwani wengine hawaonyeshi jinsi walivyo kitabia wanajibania ila DULLY ana jiachia tu au sio pia charles anajitaidi wadada kwa kweli yule wa mwanza msabato nae yuko juu anae muuguza ABDUL mda mwingi yangu ni ayo tu all the best kwa washiriki ila kuna mdada mmoja anaongea sana sijui mode anaboa kiasi flani apunguze kuongea.

Anonymous said...

Hi naitwa KEMILEMBE namupa big up sana ABDUL mshiriki toka zenj.Ebu jaribuni kuwagawa katika makundi na muwape mada hii ya janga la ukimwi wenyewe kama watu ambao tayari wana explosure wanajulikana watakabiliana nalo vp na mada nyingine ni kwamba katika familia kati ya baba na mama yupi ni kionozi wa familia wasibezi katika dini pia mtafute mada yoyote kuhusu elime ya uzazi wanajua vp mana iyo si lazima usome darasani.Au mada yoyote ya historia ya zamani jinsi mababu zetu walivyokuwa wanaishi walinganishe na sasa jioni ili waweze kudiscuss au waelezee chanzo cha makabila yao something like that.Nawatakia mafanikio meme au waulize waelezee maana ya ujasili mana kuna wenzao wawili walidondoka walipopata taarifa za kwena nyumbanu na kukaa kijijini wamejifunza nini hapo.

Anonymous said...

hi hao wanaosema mbona kamela inamlenga only abdul kwanza yuko juu ana ufahamu wa mambo mana kuna siku wliamuka wakakuta amri waongee ki ingereza siku nzima wengine walikuwa kimya siku nzima ila abdul yupo kila sehemu kidogo kidogo na watu kama hao ni vigumu kuwapata katika life hii tunayoishi umeishanifahamu hapo pia ata ukiangalia kwa makini washiriki wenyewe wanapenda abdul aongee alipo adbul haliharibiki jambo ki ivyo unacheki mana kuna dully,charles na maulid bonge wanachangia mada sana ila abdul yuko juu zaidi mana charles na maulid wanachangia ndio ila wanjifanya wastahabu flan au wanajidai unaona lakini dully anaonekana ni mtoto wa kijijini kabisa kwani tunachoangalia ni yale maisha alisia ya kijijini ndio maana ya maisha plus umeisha fahamu wenzangu ndio maana dully yuko juu mimi nitaendelea kusema dully yupo juuuuuu sanaa

Anonymous said...

HI naitwa kage wa kagera mimi namupa big up sana abdul anajitaidi kuishi kijijini kwa kweli akitoka kipindi kiatkuwa kinaboa sana ana uwezo wa kuwashawishi wenzake kama pale alivyosema niombeeni naumwa walianza kama kuzalau lakini alikomaa hadi wakamuombea yuko fresh kabisa abdul pia mje muwape kama hadithi flan au tukio flan alafu watoe coment wamejifunza nini baada ya kuangalia icho kitu au kusikiliza poa big up sanaa masudi kipanya na kaka bonda.Au jioni mukiwa mumekaa waulizeni washiriki kitu ambacho hawatakisahau hadi hapo walipo cha furaha au uzuni na amini watajifunza kitu hapo poa

Anonymous said...

HI naitwa kage wa kagera mimi namupa big up sana abdul anajitaidi kuishi kijijini kwa kweli akitoka kipindi kiatkuwa kinaboa sana ana uwezo wa kuwashawishi wenzake kama pale alivyosema niombeeni naumwa walianza kama kuzalau lakini alikomaa hadi wakamuombea yuko fresh kabisa abdul pia mje muwape kama hadithi flan au tukio flan alafu watoe coment wamejifunza nini baada ya kuangalia icho kitu au kusikiliza poa big up sanaa masudi kipanya na kaka bonda.Au jioni mukiwa mumekaa waulizeni washiriki kitu ambacho hawatakisahau hadi hapo walipo cha furaha au uzuni na amini watajifunza kitu hapo poa

Anonymous said...

Abdul mtoto wa mama saa zote kulala mapajani mwa wanawake tu, kazi hafanyi anataka alelewe na wanawake (wanaume kama mabinti) hiyo ndo tabia ya huyo mtoto wa kizenji. Arudi akanyonye maana anataka kunyonya huyo. Anapenda tu cheap popularity.

Anonymous said...

habari zenu hongeleni kwa kipindi kizuri
ila kwanini Abdul anaonyeshwa sana kuliko wemgine??????????na wala amtaki kujirekebisha au ndo mmeshamchagua awe mshindi ndo maana mnamwonyesha sana?nawafagilia MOSH NA Modesta wako juu nawatakia mashindano mema.

Anonymous said...

Habari za kazi waandaaji wa maisha plus.

Mimi ninachotaka vi, hivi kigezo cha kuwa mshindi katika ashindano haya ni mtu kufanya kazi sana kupitakiasi hadi kukosa muda wa kuongea na wenzio au ni maisha yote kwa ujumla na jinsi nzima ya kuishi na wenzio? Mie huwa nashindwa kumuelewa mshiriki mmoja anae itwa nasibu, mbona anajifanya yupo bize sana na kazi kiasi kwamba anakosa hata muda wa kubadilishana mawazo na wenzie na ninyosikia anapenda kujitenga na hata wenzie wanapomfata kujaribu kukaa nae sehemu yeye anaondoka hii inaonyesha kuwa yeye ni mbinafsi sana na hapendi kushea mawazo yake na wenzie hivyo hafai kuwa mfano kwa jamii kwa swala zima la kimaisha aondoke tu kijijini anaboa sana kwakweli.

Kitu cha pili, mimi nahisi hivi washiriki wanavyochanguana wenyewe kwa wenyewe juu ya swala zima la kutoka kijijini mimi nahisi wanachanguana kwa chuki binafsi na wala si kwa vigezo ambavyo vinastahili hivyo nilikuwa napendekeza mtafute njia nyingene ya kuwapendekeza wanakijiji ktoka kijijini eithar watanzania ndo wawe wanapiga kura za watu hao watatu wanaopaswa kuwa kwenye hatari ya kutoka au whetever lakini si kwao kuchaguana wenyewe.

ghalib shariff said...

hellooo mi naitwa ghalib kutoka mtwapa mombasa kenya
jamani mnyonge msongeni lakini haki mumpe kipaji hakipokonyeki ikiwa anae ngra ni abdul wa zenji kipenga cha mwisho ndico kitakacho tupa mshindi akili ni nywele kila mtu ana zaketuwache kumuonea gere abduli hiyo ni hulka yake waswahili wasema asiye funzwa na wazazi atafunzwa na ulimwengu maisha plus ni moja katika ulimwengu wa mafunzo masoud kuwa kidete usikubali mrungura,
maulid wadi na abduli wako juu kimahesabu

Anonymous said...

Habari ya kazi waandaaji wa maisha plus kiukweli mi nawakubali na mmeanzisha kitu bomba sana hapa tanzania mi nafuatilia kila hatua ya kipindi chenu sijaona kasoro yoyote makosa yaliyojitokeza ni ya kawaida kabisa na sio kama kumuonyesha Abdul eti ndio amepangwa awe mshindi hapana mi ninavyoona kwakua Abdul ameamua kuonyesha tabia zake hadharani na akupenda kuzificha, ndio maana maiha plus wanamuonyesha sana ili mzione. napenda kuwashauri Watanzania wenzangu tusipende kulaumu kama unamuona Abduli hafai basi mpigie kura kwa wingi mshiriki unaeona anafaa, kwangu mimi Abdul, maulid wadi, Steve wako juu, nawaombea mmoja kati ya hao ashinde. Big up masudi na Bonta nawakubali sana. Josephine G.
kihesa-Iringa

Anonymous said...

Habari zenu Masudi kaka Bonda nawapongeza sana kwa kazi nzuri ya kulea vijana hapo kijijini hakika maisha wanayoishi vijana hao hapo kijijini ni maisha ya Mtanzania halisi, ni maisha yenye ujasili mkubwa sana hakika vijana hao wakitoka huko watakuwa ni mfano bora kwa vijana wenzao Pia nawapongeza Nasibu na pendo kwa kuwa vijana wenye bidii Nasibu anaonyesha ni kijana chapa kazi hapendi majungu, kwani njia ya kujiepeusha na majungu ni kutojichanganya bigup.

Anonymous said...

Hamjambo? mimi nafanya kazi chuo kikuu,napenda kuwapongeza wandaaji wa maishaplus, vijana ninyi mnaona mbali sana, kwani mmeweza kuwakusanya vijana kutoka mikoa mbali mbali ili kuja kukaa kujijini na kujifunza mambo ya huko, hii inaonyesha ni jinsi gani mmekomaa kiakili na kimawazo, mmeweza kuwafunza mambo mbali mbali yanayofanywa hapo kijijini, kipindi ni kizuri kiendelee kwa vijana wengi. Nampongeza kijana Nasibu, pendo, Boniface kwa kazi nzuri na vijana waliotulia hongereni sana.

Anonymous said...

hellow maisha plus mimi KARIM KAWAMBWA na kaka yangu RAZAK kawambwa tupo lindi tunashangaa kwa nini wengi walienda na bibilia kwenye mbuyu na mau kwa nini hakwenda na silaha wakati yeye mwanaume angekutana na nyoka je tunamfagilia sana hamisi kwa kwenda kiume na panga na mwisho abdul anatisha ndie star wa maisha plus mkimtoa tutaandamana!

Anonymous said...

Nimekerwa sana na mlivyowatoa charls na steve, kwani modesta ana mvuto gani mpaka mnamuacha? Kazi yake kubwa ni kudeka tu sasa anamdekea nani si akadekee kwao, yaani nahisi maishaplus inaanza kupungua mvuto. Mi Baraka wa kihonda Moro

Anonymous said...

hi mimi naitwa hamza,maisha plus iko juu, ila kipindi kingine jitahidi muwe na 24hrs channel ili washiriki wapate muda wa kutosha kuonekana wanavyofanya maisha, big up maisha plus

Unknown said...

Hi maisha plus

Unknown said...

Maishaplus hongera,naomba email yenu tafadhali

Anonymous said...

Nimefuatilia kipindi chenu kwa muda mrefu, nia has ni kutaka kujua mantiki ya kuwepo kwa kipindi hiki, nimeelewa kwa sehemu,bado naendelea kukitaza ili kujua zaidi. Lakini kitu kimoja ambacho hakinifurahishi ni jinsi mlivyoshindwa kuwaandalia mazingira ama ya ajira au namna nyingine ya kuwawezesha washindanaji wanaondolewa kwa kura za wananchi namna ya kuishi baada ya hapo. Nasema hivyo kwa maana nzuri kwamba hao vijana hapo walipo wana tumia muda wao kwa malengo maalumu, kuwaacha wanapotoka ni kuwapotezea muda. Think about it positively.

Matern Kayera
Mwanza

Anonymous said...

shindano halijaisha watu washaanza kumtangaza abdul kiaina kuwa mshindi. kila mtu abdul.. toka awali halafu hata yeye anahisia tayari za kuwa mshindi. muonekano tu na face view yake inaonyesha kuwa anajua kuwa yeye ni mshindi. natambua huvo uhakika anaooo abdul. sio vema tuambieni km mlishaamwandaa huyo abdul. tusiwe tunapiga kura hewaa. ila nawapongeza wabunifu na waandaaji wa maisha plus mpo makini na akili zenu, kipindi kipo bomba ila UFISADI umeingilia kati. naitwa LIKOLO

Anonymous said...

Hi maisha plus, Mimi ni karen ni mpenzi sana wa maisha plus, kwa upande wangu naona Abdull yuko juu hata kama anaonekana sana ni kwa sababu hao wengin hajichanganyi na hawataki kuonyesha uhalisia wao. Ni hayo tuu.

Anonymous said...

Hi maishaplus kaka masoud kaka bonda, poleni kwa kazi kubwa mnayoifanya. Hongereni kwa kuandaa kamchezo kama comedy, nawapongeza sana wanaume wamefanya vizuri, walipendeza, wasichana nao wamejaribu biup, endeleeni kuwapa michezo mingine ili tuone vipaji vyao, nadhini wengi wao wana vipaji pia itakuwa vizuri kama kila mtu aonyeshe kipaji chake. A.Hussein DSM

Anonymous said...

Hongera maisha plus. mie nampenda UPENDO.Clara toka Kigali Rwanda.

Anonymous said...

hi, naomba huyo kaka anayetoka mbeya na da asha watoke kwenye mashindano.

Anonymous said...

Hi kaka bonda na Masoud
Nawapongeza sana kwa ubunifu wenu.
Napenda steve na chazi wabaki kijijini.
Pia nina wazo kuwa washiriki wasiwe wanachagua watu wa kutolewa tuachiwe sisi tunao angalia ndio tutapiga kura na wawili wakipata nyingi watolewe.
Asante Veronica wa Arusha

Anonymous said...

Dear Wandaaji wa Maishaplus, poleni kwa kazi kubwa mnayoifanya, nawapongeza sana. Nampongeza Mshiriki Nasibu kwa kuwa ni kijana anayeishi kijijini kama vijana wa kizamani,anafanya sana kazi, kuhusu ukimya wake, ninavyofahamu mimi mtu ukiwa bussy si rahisi kuanza kuongea ongea bila mpangilio, mbona inapotokea mada anachangia, mpeni nafasi anafaa. mimi peter wa DSM

Anonymous said...

Kaka bonda masoud mko juu kwa kuandaa maisha plus mimi ni mpenzi wa kipindi hiki cha maisha plus najitahidi kisinikose kama umeme haujakatika naangalia kila siku. Nampendekeza kija mmoja Nasibu anafaa sana kubaki kijiji, hata kama ataikosa hiyo millioni kumi lakini kazi kubwa amefanya hapo kijiji, nasema hivyo nikiwa na maana kuwa kijana huyo hachoki wala hachagu kazi. Mimi mdau wa kuangalia maisha plus kutoka Dar

Anonymous said...

Kaka Bonda,Masoud hamjambo poleni kwa kazi nzuri,kusema kweli kazi ni nzuri sana mnayoifanya mko juuuuuu!!!!!! Ndugu zangu naomba nieleweshe kitu kimoja jana nimeangalia kipindi chenu cha maishaplus,Napendekeza kijana Nasibu abaki kijijini kwani ni mhimili wa kufanya kazi hapo kijijini, kama mtamtoa mtakuwa mmekosa jembe kama si trekta, kwa maoni yangu muacheni mpaka mwisho hata kama hatapata hizo milion kumi ni muhimu sana kwa kazi huyo kijana

Anonymous said...

Kaka Bondi nawe kaka Masoud pia nanyi hongereni kazi mnayoifanya ni nzuri sana.bado Upendo ni kiboko yao hata Abdul amekubali na kumpa kura mwenyewe,si mliona? Clara,Kigali Rwanda 250 0788622439 or umuhocla@yahoo.com.

Anonymous said...

Hi washabiki wa maishaplusi mie nawapenda wabaki kijijini Nasibu na Asha bigup

Ray DSM

Anonymous said...

Hi Masoud, bonda hongereni, mimi naitwa A. Hussein kutoka Dar nawafagilia sana Nasibu na Asha wabaki kijijini, kama Nasibu anafanya sana kazi, waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni kijana Nasibu ni chapa kazi katika kijiji chenu, hivyo kumtoa itakuwa pigo sana, hata hivyo amechangia sana pia si mwoga kama vile alivyoshika mafuvu kwa mtu mwingine hathubutu kushika hata kwa bahati mbaya

Anonymous said...

hellow maisha plus me ningependa kumfagilia sana abdul maana ni mmoja na pekee mwenye kuonyesha tabia yake halisi na sio kama hao wengine wanajificha ficha nadhani anastahili kuchukua million kumi kwasababu ndio pekee mwenye kuonyesha tabia yake na kwangu mimi naona ni sawa tu yuko bomba!!!!!!!!!! tukitaka tusitake abdul ni tishio la wote.
mdau kutoka znz

Anonymous said...

Hi maisha plus, hebu kesho washiriki wafanye zoezi la kuwasha moto bila kibiriti wala mafuta ya taa,yaani kwa kutumia njia walizotumia mababu zetu (kupekecha)kama sikosei MAKUNDI KWA MAKUNDI
Clara, Kigali Rwanda.

Anonymous said...

Hi mimi naitwa Kamti A.H wa Geology UDSM, nawapongeza waandaji wa kipindi cha maishaplus, Masoud, Bonda hongereni sana kwa kazi nzuri. Naomba kutoa maoni yangu. Nadhani ninyi ni vijana mliopevuka kimawazo na kiakili na ndio maana mkamua kuandaa kipindi hiki cha maishaplus kwa vijana. Hivyo basi nawaomba kwa jicho la huruma wale wote waliotoka muwawezeshe angalau kuangalia vipaji walivyonavyo kuwaendeleza, kwani mliopokuwa mnawachagua huko mikoani kuna kitu ndani yake mlikiona walichonacho vijana hao walioingia kijiji na wakaishi huko mpaka kutoka kwa kupigiwa kura, sio kwamba hao waliobaki wana uwezo mkubwa kushinda wenzao waliotoka la hasha hiyo ni game. Hivyo basi ili kuwasaidia fanyeni kitu ambacho hata Dunia itawapongeza kwa kuwatoa vijana hao italeta changamoto sana. Nadhani mtaweza, kwani nia mnayo na uwezo mnao nawatakia kila la kheri.

Anonymous said...

Maisha plu iko juu, nampenda Nasibu amabaki kijijini mpaka mwisho, anafanya kazi sana na ni mpole, hana majungu wala makuu ametulia

Naitwa Charles kutoka DSM

Anonymous said...

Hi waandaji wa maishaplus, jamani msimtoe Nasibu Mpangala kwani anao uwezo mkubwa ni chapa kazi sana hapo kijijini, ni mpole hana kelele yeye kazi tu kweli anaonyesha wakijijini, kwani watu wa kijijini huwa hawakai kijiweni na kuchonga chonga sanaaaaa wao ni kazi baada ya kazi kula kunywa pombe za kijijini, nani halijui hilo? mpole wake ndivyo alivyo hataki majungu. Nawatakia kazi njema. Mimi Hashimu kutoka Kinondoni DSM

Anonymous said...

Hi Masoud, kaka bonda, hongereni, pamoja na hayo wafikilieni mnaowatoa kwa kupigiwa kura kwa kuwaendeleza kwani wapoteza muda mwingi na shida za kijijini, waoneni huruma, ninyi vijana ni wabunifu hivyo muwawezeshe vipaji vyao, jaribu kukaa nao na kuwashauri nini wanaweza ili nia na Dhamira yenu ya maishaplus ipate sifa. Msiwatelekeze hivi hivi wapeni kazi za kufanya, hilo nina uhakika mnaweza sana, kama mmeweza hili halitawashinda hilo.

Kazi njema, A.H. DSM

Anonymous said...

hiy naomnba chaz na steve wabaki kijijini

Anonymous said...

Mchezo ni mzuri ila hamkuonyesha uhalisia wa maisha ya kijijini kama matumizzi ya maji ya kopo haikuwa lazima ,wangetumia maji ya kawaida hapo wangefunza jamii kuchemsha maji ya kunywa.juisi wangetengeneza za matunda halisi.muda wa kipindi uongezwe.Naitwa PATRIC MASAGA

Anonymous said...

Hellow,hongereni sana kaka Masudi na huyo mwenzako,nampongeza sana Steve, Charles,Abdul na Upendo.Jamani naomba Steve na Charles waendelee kubaki kijijini.

Anonymous said...

Hi Kaka Masoud na Kaka Bonda,tafadhari msiwatoe Nasibu na Asha kwani wanofaa kubaki kijijini.wanachapa kazi na si wabishi.

Clara. Kigali, Rwanda.

Anonymous said...

Hongera sana kaka Masoud na kaka Bonda,vipi kuna watu wanakera sana katika maisha plus has modesta wanangoja nini wasitolewe, namfagilia sana Abdul na Maulidi nataka mshindi achanguliwe kihalali si kwa upendeleo, wala elimu ya mtu,


Mama Hassani Shaw , Keko Bora

Anonymous said...

Mambo kaka Masound, ulikuwa wapi toka zamani hukuazisha mambo haya, kwani unawapa changamoto sana vijana, wanajua nini wafanye katika maisha tofauti ya kidunia, pia wanajua kuna kupata na kukosa, kuna raha na shida,
hakuna mtu anayeniuzi katika maisha plus kama pendo anajifanya yeye ni mjuaji wakila kitu kwa vile ni msomi twataka mshindi atoke kihalali si kisomi.

Hidaya Ramadhani - Keko Bora

Anonymous said...

Hii, Kaka Masound na kaka Bonde, mnyonge mnyongeeni haki yake mpeni Abdul anatisha tena sana hayo mengine anyoyafanya ni vichocheezi tu vyakufurahisha watazamaji na kukifanya kijiji cha maisha plus kilete burudani kwa watazaji wasichoke kukitazama nahisi bila vituko vya Abdul watu wasingependa kukitizama kipindi cha maisha plus, Mpeni hizo 10,000,000/= zake msimbanie na kutaka wasomi


Mama Shaw - keko Bora

Anonymous said...

Maisha plus iko juu, Abdul we acha tuu, anatisha


Anastasia Kilonda - Tabata Bima

Anonymous said...

Hi,ila Upendo anaboa,ushindi achukue Abdul
Clara Kigali, Rwanda.

Anonymous said...

Huyu Upendo kaonyesha tabia mbaya sana.Pia Teddy na Modesta.Kwani hawana uhakika na maneno yao ya kusema eti Abdul ni mchawi.Sio ukweli hii inaonyesha jinsi Wasabato na walokole wanavyoshuhudia uongo.
Wameonyesha reality ya hizi Dini kushuhudia uongo hawana ukweli na wayasemayo.Upendo kwa sasa hawezi pata hiyo mil 10.wakupewa bado hajajulikana kwani siku ya siku mambo yanabadilika.

Mdee wa Arusha

Anonymous said...

Hivi kwanini huyu Pendo anafanya vitu vya ajabu mnamuachia?anakifanya kipindi chenu kionekane hakifai katika jamii, haya mambo ya uchawi yanatokea wapi kwanini hapo mwanzo yasiwepo yajeyaonekane mwishoni zote hizo ni fitina tu za kutaka kumchafulia abdul jina, kelele anapiga yeye pendo peke yake mbona wasichana wenzake wametulia, inabidi kamera yenu ijitahidi kuonyesha vitu vitakavyo wapendezesha wananchi sio vitu vingine ambavyo havina maana kabisa, km hirizi au mambishano ya uchawi, nasema pendo ameniuzi sana na naomba kaka Masoud na Bonde mumchukulie hatua kali ili asikitie dosari kipindi chetu cha maisha plus


Mama Ushauri wa Keko

Anonymous said...

masoud umedhihirisha ni jinsi ganiuna upeo mkubwa sana wa kufikiria. haiwezekani mtu arogwe kwa hirizi. kwa mtazamo wangu na hasa baada ya kuona sura za akina pendo, modesta na ted mara baada ya kubanwa kwamba hirizi huvaliwa mwilini kwa hiyo ni lazima ile ni ya msichana na hasa kwa vile imekutwa kwenye choo cha wasichana ni wazi ile hirizi inauhusiano na mmoja kati ya PENDO, TED NA MODESTA. abdul big up yupo juu

Anonymous said...

Hai to ALL,
Nawatakia kila mema yote katika safari yenu yakutafuta milioni 10.washiriki wote wako fit kinoma lakini Teddy pamoja na Mzee Kikwete wanatisha nawafagilia saaaaaaaana,bila hao kipindi hakinogi.
Nawaambia washikaji kazeni buti uwanja niwenu na milioni kumi nizenu.
Regards,
Godian Mukuru
Julius Nyerere International Airport
Dar es salaam-Tanzania.

Anonymous said...

I LIKE THE GAME! IT'S EDUCATIVE AND MUCH MORE BRING A PERSON INTO CREATIVE CHALENGES! BIG UP ALL THE FINAL TEN PARTICEPANTS..... MKO JUU SANA ILA, PENDANENI...ILI MFANIKIWE KATIKA KILA MTENDALO!

Anonymous said...

Hi people
Napenda sana kufuatilia kipindi cha maisha +, tangu mlivyoanza kurusha vipindi hivi kweli mmetufanya sisi watanzania tuvutike sana na vijana hawa wanavyoonyesha maisha halisia ya Kijijini (Kitanzania), kadri muda unavyokwenda ndio hao vijana wanazidi kuonyesha upeo walionao na uwezo wa ku handle mambo katika maisha ya kila siku, Binafsi nawapongeza sana waandaaji wa Maisha +, real walifikilia mbali sana na hii inaonyesha kuwa watanzania wa leo c wale wa jana, BIG UP SANA 2 U PEOPLE.
Its me James.
Documentary Lab Makole-Dodoma

Anonymous said...

Hi kaka Masoud na Bonda, mmefanya vizuri sana kuwakutanisha hao washiriki na kuzunungumzia swala la Hirizi. na hapo Abdul atajisikia amepunzika kwani ilikuwa kama amechukua mzigo wote yeye.pia nampongeza Abdul kwani alionyesha uvumulivu wa hali ya juu.
Clara Kigali, Rwanda.

Anonymous said...

mi natokea arusha,na nimefuatilia sana kipindi cha maisha plus toka kimeanza,nawapenda washiriki wote hamna aneboa wal kuharibu kipindi,nikwamba watazamaji lazima waelewe kwamba nini ya maisha plus alafu ndio watoe dosari za haovijan wenzetu waliopo hapo kijijini,bila pendo kuchonga,au at wakigomban hayo yatakuwaje maisha plus yani haou vijan wanaonyehsa maisha halisi ya binadamu katika jamii,kugombana kupo,kusingiziana kupo so bila hayo mambo maisha ukijumlisha yatanogaje?na kwa sababu hu ni mchezo lazima watu waotke na ni kwamba kila mtu anataka kubaki kwa hiyo lazima amtaje mtu ili ajililie nafsi yake,nawashauli watazamaji wao wamchague mtu wanae muona anfaa kupat hiyo millioni kumi lakini siyo kusema fulani ni mchawi,fulanni,anamdomo kwani kila mtu anamdomo na ushirikina waafrica tupende tusipende tunao
G.A from arusha