22.11.13

Thursday, June 24, 2010

TUKAINGIA ZIWA VICTORIA KUVUKA KWENDA UPANDE WA PILI.

Hii sehemu kwa huku Mwanza inaitwa FERI, niliambiwa sehemu hii ndio wananchi wanavuka kwenda upande wa pili, kwa wale wanaokwenda Geita na sehemu nyingine hupitia njia hii.

Sehemu inavyoonekana kabla hujaingia unatakiwa kulipia kila mtu shilling 300, na gari linalipiwa shilling 700

Hapa tuliambiwa tushuke wote kwenye gari na tuingie kwenye boti, sasa bwana kumbe kuna watu wanaogopa kuvuka na maji.
Mida ilivyokuwa inakwenda majamaa fulani walikuwa daaaah hadi unawaonea huruma, majina tuyaweka kapuni

Marco Chali aliyekaa katikati akiwa na wadogo zake wawili.

Tulipishana na boti nyingine ikiwaleta upande ambao tulitoka sisi

Upande wa pili ukionekana hivi.

Tukaingia GEITA salama na usafiri wa huku wa fastafasta ni huu hapa kama unavojionea mwenyewe.

2 comments:

Ima (The Designer) said...

Mzee Safari imetulia sn, hapo unapata experience la nguvu ktk maisha na safari na pia ss tunaotembelea blog pia tuna pata somo muruwaaaaaaaa, mm nawatakia kila la heri ktk safari yenu.

Unknown said...

Huko ndiyo kanda ya ziwa raha kwenda mbele, matunda, samaki, kuku wa kienyeji, mpunga wa kunukia, miwa, na watu wakarimu, dhahabu sasa usisahau kuleta japo tolla moja kaka