22.11.13

Friday, June 25, 2010

WATU WA MIKOANI MPAKA WAKUONE NDIO WANAKUJA KWENYE SHOW.

Huku vijijini bwana kama unataka ujaze ukumbi lazima wasanii uliowataja wazunguke kila kona ya mitaa ili wananchi waweze kuwaona na kuamini kwamba kweli wale waliotajwa ndio wanaoimba siku hiyo.
Kama unavyoona gari la matangazo likiwa na spika na wasanii wanatakiwa kukaa kwenye chuma ili waonekane, hela bwana

Wakati tuko barabarani Chege na Mh Temba walikuwa wanauza tisheti zao kwa wananchi, gari linasimamishwa na biashara inaendelea.

Hapa tulipita ni stendi kuu ya mabasi Geita ikitengenezwa

Watangazaji kutoka Geita walikuwa ni hawa.

Ilikuwa tukifika sehemu ya watu wengi tunasimama na wasanii walipewa MIC na walikuwa wakiongea na wananchi.

Hapa ndio sehemu wanayotoa mchele kwa wingi.

Soko kuu la Geita

Watoto wengi walikuwa wanamuita Chege kila tukipita

1 comment:

Anonymous said...

ithink thats the really adver sio unapeleka jina tu watu wanataka kuona vitu live,i like this style jamaa sio mabrathamen huko ndio kuzichanga
mdau south korea
jeremia