22.11.13

Wednesday, July 28, 2010

"HUU NI WARAKA WANGU KWA WASANII WA MZIKI KABLA YA UCHAGUZI MWEZI OCTOBER"

Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi october mwaka 2010,huu ni waraka wangu kwa wasanii wote wa mziki wa kibongo!. Najua kuna miaka mingi sana ya kuukomboa huu mziki wetu lakini wazungu wanasema "One step at a time"...na muda ndio huuu..........!!!!

Miaka kibaao sasa wasanii mmekuwa mkilalamika juu ya kudhulumiwa haki zenu kwa kuibiwa kazi zenu na kulipwa malipo madogo ya album zenu kiwango kisichokidhi mahitaji yenu,hilo ni sawa kabisaaa!!

LAKINI je!! mmejipanga vp kumaliza hili tatizo lenu? kila kukicha viongozi wanawa-ahidi kwa mdomo kuwa watamaliza tatizo lenu bila utekelezaji wa vitendo kitu ambacho mimi nakiona kama ni kiini macho na nyinyi wenyewe mnakifahamu....

Viongozi hawa hawa ambao wanakataa kwa "makusudi" kusimamia maslahi yenu ndio hao hao wanaokuwa wa kwanza kuwachukua nyinyi wakati wa uchaguzi ili muwasaidie kuwapigia kampeni kwa kutoa burudani pindi wanapokuwa kwenye mikutano yao,,,,

Sasa inakuwaje mnatumika kirahisi namna hii? wakati kwenye interview zenu wengi wenu mnajinadi kuwa nyinyi ni wanaharakati na sasa mnafanya mageuzi ya huu mziki wenu,vp mageuzi ndio haya? Mnapotumiwa kwenye kampeni mnacheka cheka kwa furaha pale mnapopewa laki kadhaa au vimilioni kama shukrani ya "kinafki" kutoka kwa hao watu waliowatumia!!!! Na baada ya kumaliza kampeni zao hao hao wakiwa madarakani wanawasahau na kujifanya hawawakumbuki tena hadi wakati mwingine wa uchaguzi.....(huu ni utumwa wa kifikra) najua mtasema mnaangalia pesa na ndio mana mnawafanyia kazi yao na sio kitu kingine!!! Sawa sikatai huenda ni kweli pesa ndio mnayofuata,,, sasa je? nyie wasanii wa kiume ikitokea wamama wakiwapa pesa za kutosha na kuwataka mkatumbuize kwenye "kitchen party" yao mtaenda kudhalilishwa sababu ya pesa au mtakataa?

Sidhani kama ntapata dhambi nikisema kuwa kitendo cha wasanii kutumiwa kwa muda na hawa watu mi nakifananisha na binti wa kike ambae bwana wake huwa anajifanya kumjali na kumfuata pale anapotaka penzi lake tu!! na akishamaliza shida zake anaondoka na kumuacha binti huyo akiteseka na hali ngumu ya maisha bila ya msaada wowote na hurudi tena pale anapokuwa na shida hiyo!!

Enyi wasanii kwanini mnajipa thamani ndogo kiasi hicho???
Huu ndio wakati wenu wasanii kuonesha mapinduzi yenu na misimamo yenu na zile harakati ambazo kila kukicha mmekuwa mkizitaja kwenye nyimbo zenu na interview zenu,,,yawapasa kudai maslahi yenu kwanza kuliko kutumika kuhangaikia maslahi ya watu wengine....

Sitoona ajabu nikiwaona wasanii wale wale wanaokuwa wa kwanza siku zote kudai haki zao wakitumika kwenye kampeni mwezi october na kisha baada ya uchaguzi mwakani wasanii hao hao tutawaskia tena wakilalamika kutokumbukwa na viongozi husika!!!

"CALCULATE THE RISK,BEFORE YOU JUMP"
By Mtoto wa vitoto..
(Ze' son of babiez)
2010...

4 comments:

Daniel .E. Simfukwe said...

daah hii iko deep sana Mtotot wa vitoto

Anonymous said...

Matatizo ya wasanii hayana uhusiano na chama chochote cha siasa. Inawezekana wahusika ni wafuasi wa vyama tofauti na ni haki yao ya msingi kuchangia vyama vyao. Imefikia hatua kila tatizo tulilo nalo tunalifanya la kisiasa na ndio maana tunashindwa kutatua matatizo na kuishia kulalamika tu. Huu wizi wa kazi za wasanii haufanyiki Ikulu au bungeni Dodoma.

Kama mnao ubunifu wa kutunga nyimbo za mapenzi na jamii ikazikubali. Tumieni ubunifu huo huo kuwashawishi watanzania wanunue kazi halali za wasanii.

Anonymous said...

Kaka umezungumza, tatizo wasanii wetu ni ukosefu wa malengo na maisha, msanii yupo tayar kupokea laki tatu leo na kukosa laki tatu kila mwisho wa mwez,sidhan kama umekuwa ni ulimbukeni wa kushika hela na kusahau unachokipigania kwa maisha yako.. jaribu kutizama wale waliotumika 2005 wapo katika hali gani bila kusahau hao waliojifanya wamealikwa kuzungumzia maslahi yao na wasanii kwa ujumla.. wanajitahid kuburudisha lakin kauli itabaki ileile kwamba kuwa msanii Tanzania ni baada ya kukosa la kufanya hii yote inatokana na uhalisia wanaouonyesha kwa jamii inayo wazunguka

mmeshindwa kujitambua sasa jamii itawatambua vipi

Anonymous said...

Kuna makala mbili hapa ambazo zinazungumzia haya matatizo:

http://vijana.fm/2010/07/27/ze-utamu-arudi-kuwapangusa/

http://vijana.fm/2010/07/21/vijana-wa-tanzania-tuamke/

Zisomeni halafu mfikirie mambo kwa kina.

Nawasilisha.