22.11.13

Friday, September 10, 2010

BAADA YAKUTOKA MJENGONI NIKAELEKEA MOJA KWA MOJA STUDIO

Baada yakutoka Clouds FM nikaelekea moja kwa moja hadi pale maeneo ya Mlimani City palipo na studio inayokwenda kwa jina la NGOMA REC chini ya Producer Tuddy.
Hapo ni kwa nje kwa jinsi inavyooneka

Nikaingia ndani ya studio na huyo aliyekaa hapo ndio producer mwenyewe anaitwa Tuddy, nyimbo hit alizotengeneza ni pamoja na
Bembeleza ya Marlaw,
Zai ya Soggy Doggy,
Natumaini ya Beka, Barnaba na Amin,
Pi Pi Pi ya Marlaw,
Unikimbie ya Amin,
Heyeeh ya Nash,
Mama Halima ya Linex,
Pombe ya Mwasiti,
Wabishi wa Town ya Soggy, Dnob, Chidi Beenz,
Mr. Bottion ya B.O.B Click.

Ilibidi msanii Ditto aingize mistari yake fulani ili kumalizia track yake mpya.

Linex naye alikuwepo ndani ya nyumba kukamilisha vitu fulani fulani, wimbo mpya alioutoa Linex unaokwenda kwa jina la mama Halima umetengenezwa katika studio hii ya Ngoma.

Mtu mzima niliombwa nipige chata katika picha hii ili kuweka kumbukumbu kama nilipita na mie hapa safiiiii....

Jamaa walipomaliza kuweka mambo yao sawa tukaamua kusepa kwenda kuianza sikukuu vizuri
Eid Mubarak ndugu zangu.

No comments: