22.11.13

Thursday, September 09, 2010

MIMI SINYWI POMBE, WALA SIVUTI BANGI "Madee"

Jana kwenye kipindi cha XXL kinachorushwa na radio ya Clouds FM na kuendeshwa na mtangazaji B12 ilikuwa ni siku ya DISS DOT COM.
Diss zilizosomwa zilikuwa nyingi lakini diss iliyo make hard line ni pale msikilizaji anayekwenda kwa jina la Chitemwe kutoka Tabata alipomdiss msanii kutoka TIP TOP anajulikana kwa jina Madee na kumwambia kuwa anaboa anapokuwa stejini amekunywa au kuvuta bangi so anapoimba anakuwa amelegea na hafanyi vizuri stejini.

Sasa leo mtu mzima Madee akashuka mjengoni Clouds FM na kumjibu jamaa huyo aliyetuma diss hiyo namnukuu
"Mimi nilikuwa studio pale kwa master jay na wenzangu nikapata simu zinazosema kuwa kuna mtu kanidiss kuwa mimi mlevi hadi nikiwa stejini nawaboa mashabiki, kilichoniuma zaidi hadi mama yangu alinipigia simu wakati huwa asikilizagi radio. Nachopenda kumwambia huyu kijana ni kwamba mimi huwa Sinywi, Sivuti Bangi wala situmii kilevi chochote, sasa nachosema naweza kumchukulia hatua maana kuna vitu fulani kanipunguzia katika maisha yangu"

So kilichofanywa leo na B12 kumfungia huyo jamaa Chitemwe kutotuma tena diss zozote hadi mpaka pale aruhusiwe.

2 comments:

MloMmoja said...

B12 alitakiwa amtafute uyo Chitemwe athibitishe kauli yake, na kama akishindwa amfungie, japo haimake sense coz mfumo wa kutuma ujumbe haumpi authority B12 labda aseme hatosoma msg zake,.je atajuaje? au hatosoma msg zinazomdis MAdee?
Choka mwana!kuna kipindi tulikuwa tunaipata CLOUDS Fm live kupitia bongo5.com,.mbona sasa ivi hatuisikii tena?

Anonymous said...

mmh mnamuonea jamaa (chitemwe) jamaa ameacha lini kuvuta bangi na kunywa au mmemban tu.fanyeni uchunguzi then ndo mtoe ban ni mawazo