Muda mchache uliopita msanii wa kizazi kipya kwenye bongo hip hop ROMA amepata ajali mbaya barabara ya Morogoro. Roma anasema alikuwa yupo kwenye mwendo wakawaida ndio tairi la mbele lilipopata pancha na ndipo gari likaacha njia yake na kwenda kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha Roma kurudi lilipotokea.
Roma ananiambia kwa sasa anaelekea Hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.
Roma akimwelezea police wa usalama barabarani kilichotokea mpaka kupata ajali hiyo mbaya.
Huyu ni mmoja kati ya marafiki wa Roma aliyekuwa nae kwenye gari wakielekea Morogoro kwenye show
7 comments:
POLE SANA ROMA TUSHUKURU MUNGU HAKUNA ALIEUMIA. MDAU DODOMA
oh pole sana jembe letu roma
daa thenx God coz jembe yupo fine.. polee sana mzazi....
Pole xana' djembe
pole sana jembe tumshukulu Mungu mpo wazma wote
Pole sana roma
dar..hii noma !!!!
Post a Comment