Mkurugenzi wa VISION RECORDS Aldo Sanga
amesema mwishoni mwa mwazi oktoba mwaka huu atafanya uzinduzi wa Studio
hiyo ya Kurekodi ambayo ipo Mkoani Njombe Wilaya ya Makete.
Katika uzinduzi huo utaambatana na kutafuta vipaji ndani na nje ya Wilaya kwahiyo kama unakipaji furusa niyako unachotakiwa ni kununua form ya kujiunga kwa Tsh 10000/= tu na form zitaanza kuuzwa mwishoni mwa mwezi Septemba 2012 hadi tarehe 20 Oktoba 2012
Mchujo wakuwapata vinara utaanza mara baada ya kurejesha form za kujiunga,majaji watatoka sehemu mbalimbali kama Dodoma,Iringa na Njombe - Makete aidha watu watatu tu ndio watakao rekodi bure na kazi zao zitasambazwa na kusimamiwa na kampuni hiyo.
Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro na shughuli nzima itasimamiwa na kituo cha Redio Kitulo Fm cha Mjini Makete.
T-shirt za
kampuni zitapatikana siku hiyo kwa bei nafuu, Uzinduzi utafanyikia
katika ukumbi wa Fransic G.F.C.atakae taka kudhamini shughuli hiyo;0765 255 560/0653 255564
1 comment:
Hii kitu ni kareee aseee huyu jamaa amejipanga kw kweli sio mchezo
Post a Comment