Jina lake la kisanii ni Maua Sama, Msanii
chipukizi kutoka Moshi Tanzania. Akiwa Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza katika
Chuo Cha Ushirika na Biashara Moshi, kwa mara ya kwanza anasikika katika
kipindi hiki “Exclusively” katika nyimbo yake ambayo amemshirikisha MwanaFA
ikiwa ni nyimbo inayomtambulisha katika ulimwengu wa muziki wa Kizazi Kipya
Bongo. Ni Almasi Mchangani ambayo imegunduliwa na MwanaFA baada ya kupata
‘demo’ yake ambayo alifanyia studio za Moshi na kuipeleka mbele ya “Management
Team” yake Lifeline/T.I.A ambao moja kwa moja wakamchukua. Maua anafanya kazi
chini ya uangalizi wa Lifeline/T.I.A Inc; Label ya Muziki ambayo inasimamia
kazi za muziki za MwanaFA, amefanya nyimbo yake “So Crazy” kwa Producer Marco
Chali wa MJ Records akimshirikisha MwanaFA. Mipango iliyopo ni kumfanya Maua
Sama akawa ni mwimbaji bora wa muziki Tanzania.
9 comments:
E bhana choka ee huyu du anaimba noumah yaan,Hili n din mchangan haitaj promo vocal lake linauza sana mzee.Kwa wale wote wanaopenda good music nahic tunaanza kupata kile tunachokitaka
ni nomaaaaa..ila hii nyimbo ndo ile ya kwanza aliyofanya na "Throneboy"?
Anajua
dah jembe langu la ukweli maua to muccobs keep on hustle ma dia sister ntakusupport forever.oya choka ee right decision kumwona maua kweki anaimba,is hot.kiukweli.jah bles her
For the first time tz tumepata mwanadada mwenye vocal za kweli
Great stuff!!
Huyu mdada ni noumer..wnaojiita ma-star wajipangeee...!
Hii ni Version ya pili. ya kwanza alifanya na jamaa anaitwa "Throneboy" jamaa aliua kuliko FA. kiukweli. ukiisearch hiyo track iko huku huku kwa DjChoka. Throneboy kamfunika MwanaFA.
dj choka kiukweli uyu dada nimempokea vilivyo na amenibamba ile mbaya na saut yake
Post a Comment