22.11.13

Friday, April 19, 2013

(News) Soma barua hii ya wazi kutoka kwa mdau wa muziki nchini "MAFISADI WA MUZIKI:

Walio wengi wamezoea kusikia ufisidi katika siasi, viongozi waliokua na
uuzo wa tabia na kujilimbikizia mali chungu nzima. Ufisadi hauishii
kwenye siasa tu bali kuna ufisadi kila sehemu, kwenye kazi, mashirika
binafsi, michezo na hata katika tasnia ya muziki. Ufisidi katika tasnia ya
muziki upo, tena mkumbwa na si rahisi kuusikia wala kuuona hata
ukiwa msaani.

Swala hili la ufisadi katika muziki tumekuwa tukilifatilia kwa muda sasa
kama wadau wamuziki na tumefanya uchanguzi wa kina sana kwa
kuongea na watu tafauti tafauti katika mziki, wasanii, maproducer, ma
presenters, ma dj na wadau wa mziki.

Tumekua tukisikia malalamiko mengi sana ya wasanii hivi karibuni
kwanini nyimbo hazipingwi? Kwanini hawapati show? Na maudhi
mengine mengi. Hivi sababu nini hasa ? Nyimbo zao ni mbaya?
Hawana vipaji au? wasanii kama chidi benz, lady jd, ali kiba, bushoke,
prof jay, matonya, makamua, qchief, TID, na wengine wengi. Kuna
jambo hapa japo kua wengi hawataki kulizungumzia kwa kuogopa au
labda kwa ufahamu mdogo. Nyuma ya yote haya kuna mafisadi,
hawa ni watu ambao wanaupeleka mziki wanavyotaka wao kwa
kujifanya kama wao ndio wamiliki wa huo mziki na kutumia nafasi zao
za kazi vibaya kwa manufaa yao binafisi bila kujali mustakabali wa
tasnia ya muziki.

Kuna kijikampuni kinaitwa OSATA ambacho kazi yake kubwa ni
promotion, publishing na usimamizi wa wasanii tafauti tafauti kwa njia
ya mikataba mifupi mifupi. Wamiliki wa kampuni hiyo ni Babu Tale, Said
Fela na Suka Othumani Suka, OSATA ni ufupisho wa majina haya
matatu. 

Herufi O katika OSATA ni Othuman suka ambaye ni mfanyakazi wa
cloudfm kwenye upande wa kusikiliza /kuhakiki nyimbo za wasanii na
kuzipitisha kabla ya kupigwa.

Na herufi SA katika OSATA ni said fela ambaya ni meneja wa kundi la
Tmk Wanaume family ,

Herufi za mwisho TA katika OSATA ni Tale ambaye pia ni manage wa
kundi la Tip Top connection.

Kazi kubwa ya kampuni hii ni kusambaza muziki kwenye redio,
television, mitandao ya jamii na sehemu nyingine nyingi. Kampuni hiyo
haiishi kwenye kusambaza tu bali inafanya promotion ya hizo kazi
walizosambaza kwa kutumia pesa au lugha nyingine fasaha rushwa.
Rushwa kwa maana kuwapa mapresenter na madj wa redio tafauti
tafauti pesa kupiga hizi nyimbo wanazozipromote. Katika uchunguzi
wetu kampuni hiyo inamtoza msanii kiasi cha shilling mil 3 kusambaza
na kufanya promotion ya nyimbo. Kwa haraka haraka unaweza
kusema hakuna tatizo, OSATA inafanya biashara tu na hakuna ofisadi
wowote ule unaendelea. Katika shughuli hizi za promotion ya nyimbo
katika redio na television, OSATA huwalipa madj na wafanyakazi wa
media kupiga kazi zao na pia kuwashawishi kutokupiga kazi za watu
wengine ili wapate wateja wengi katika kampuni yao.

OSATA inamtandao wa wanahabari nchi nzima, wafanya kazi hawa
wa redio na television hulipwa ilikupiga video na nyimbo zaidi ya
kawaida. Tatizo linakuja pale ambapo nyimbo mbaya inapewa nafasi
na nyimbo bora haipigwi kabisa kwasababu OSATA imelipia promotion
kabambe. Kibaya zaidi ni pale mfanyakazi wa redio anapokua ni
mmoja wa miliki wa kampuni ya usambazaji ambae ni Suka Othumani
suka, unafikiri kutakua na haki kweli kwenye upangiliji wa nyimbo
kwenye ratiba ya redio? Unafikiri nyimbo yako itapita kweli kama
hujalipa kwa OSATA ili ufanyiwe promotion? Sanaa inakuwa vipi kwa
hali hii? Lazima msanii alalamike kwa hali hii kwababu huwezi kupata
show bila muziki wako kusikika. Huwezi kuendesha maisha kama hupati
angalau show moja katika mwezi, unaposikia msanii kaingia katika
madawa ya kulevya msimcheke tu bali kuna mambo mengi katika
muziki yanachangia kumpoteza msanii na hili ni moja wapo.

Operesheni za OSATA zinaendeshwe kisiri siri sana na wamiliki
wanaotambulika ni babu tale na saidi fella, huku wakimtaje othumani
wakijuafika jina hilo halitambuliki kwenye umma.

Angalia interview hii
kwenye youtube ya kipindi cha sporah babu tale akimtaja othumani
na saidi fella
40. Katika interview hiyo babu tale anaizungumzia OSATA jinsi
invyofanya kazi na redio/TV.

Jina hili la othumani limetumika ili isijulikane kuwa huyo mtu ni suka
othumani suka ambaye ni huyu hapa katika facebook account

Osata inatumia nyundombinu za clouds FM na Television kufanya
promotion hizo za mziki kupitia mgongo wa suka . Mikutano ya OSATA
hufanyika THT (Tanzania House of Talent) na office za cloudfm, ukifatilia
kwa karibu unaweza ukadhani OSATA ni operesheni ya redio hiyo,
mameneja hao hujichanganya kama wafanyakazi ukiwaona unaweza
usiwatafautishe na wafanya kazi cloudsfm.
Sisi kama wadau wa muziki baada ya kufanya uchunguzi wa kina
tunaamini kabisa hii ni kazi ya ruge mutahaba baada ya kuona
Tanzania fleva Unit imefeli na kujiondoa katika picha mbaya katika
tasnia ya muziki. Osata nikama chombo ambacho kinatumika tu na
THT/Ruge Mutahaba kucontrol muziki na media nyingine kwa ajili ya
manufaa yake binafsi. Kila show utakayoenda lazima umkute, mwasiti,
linah, barnaba, chege, made, tundaman, n.k – haimanishi kua hawa ni
wasanii bora Tanzania bali ndio wanaosambaziwa kazi zao na hili kundi
la mafisadi. Akitokea mtu mwingine anayejifanya anasambaza na
kufanya promotion anazimwa haraka sana kwa fitna na mipango ya
osata.

Osata imefika mpaka mmalaka ya kuwaambia ma presenter
wasipinge nyimbo ya baadhi ya wasaanii hapa nchini kwa lengo la
kuwapoteza ili waende kulipia promo. Kila mtu analia kivyake ila
hamna mtu anayetaka kuongelea ukweli kwa kuuogopa ,Osata, ruge,
THT and Cloudfm. Hii media house ilipata stress kubwa sana kipindi cha
Bwana Sugu na Anti-virus, kulikua hamna amani mjengoni hata
mahudhurio ya matamasha hayakua mazuri. Kwa kutumia njia zake za
kifisadi ruge mutahaba akaweza kuuzima moto- akaihusisha serikali
kwa kumpeleka sugu bungeni ili wapate suluhisho, kumbumbukeni
mnachezea maisha ya watu, mnaharibu kazi za watu, kujifanya nyie
ndio wamiliki wa muziki mtakuja kuumbuka vibaya sana mbele ya haki.
Hii tahadhari kwa vituo vya redio, television, magezeti na vyombo vya
habari vyote kuwa kuna ofisadi unaendelea, hili hundi na washiriki
wake wanatumia pesa kuendesha vyombo vyenu. Fanya uchunguzi
wako binafsi utaona mwenyewe, kabla ya matamasha makubwa
utaona video na nyimbo flani za wasanii flani zinapigwa kweli na ndio
hao hao utawakuta kwenye matamasha. Osata, ruge, cloudsfm na tht
nia yao ni kuucontrol muziki. Sisi kama wadau wa muziki tunasema
haiwekani kabisa.

Huu ni ufunio wa kwanza tu tunaendelea na uchunguzi, kuna nyaraka
nyingi zinakuja na tutaziwakilisha kwa jamii zikiwe zimeambatana na
interviews. Joseph Kusaga moto unaanza tena huu usije ukatoa
lawama tena, hakuna atakayekusikiliza mara hii sababu unawaachia
vijana wanafanya ufisadi kwenye ufalme wako. Kama ulikua hujui basi
natumia umeujua ukweli.

Shukrani.

3 comments:

Unknown said...

eeh bwana safii sana,..huo ndo uzalendo na ndio upendo,.keep it up meen

Anonymous said...

Who is Ruge by the way,mbona wanamuziki huyu mtu anawapelekesha sana?Au kwasababu ana urafiki na JK?

Anonymous said...

Siku kadhaa zilizopita nimeona tweet ya Jide anasema anaamin Mungu si Ruge wala Kusaga.