22.11.13

Friday, May 31, 2013

(News) YAH: MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA


Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya Maziko.
Kusafirisha mwili wa marehemu pekee ni dola za kimarekani elfu sita gharama hizi zimetolewa na Clouds Media Group lakini vilevile kampuni ya Bongo records na Push Mobile kila moja imetoa shilingi milioni tano, EMasters wametoa Tenti 20,viti 1500 na gharama za uwanja wa Leaders pamoja na Mabasi Madogo aina ya coster 5 , Miraji Kikwete ambae yeye amejitolea  kuprint tshirt 200 kwa familia na kamati, Samaki samaki wametoa Milioni Moja na Laki tano,skylyte Band wao wametoa gari ambalo litaupokea mwili wa Marehemu na kuusafirisha mpaka Morogoro,

Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:

Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738

Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB

Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanguliza shukrani za dhati

2 comments:

Unknown said...

Bro dj choka umemaster hiki kitengo cha habari.me kutoka kilimanjaro naanza kuamasisha watu 2tume michango kupitia hzo namba tayari nshaz copy in ma phone.kwa mungu kila k2 knaezekana 2tafikia hcho kiwango.shukran kwa hayo makampuni.. .ni dj mac lee from Muccobs Moshi.

Ndalama Art Gallery said...

With all respects tumekuelewa kaka, nami ntasaidia kuhamasisha watu kujitolea mochango. R.I.P Mangwair