22.11.13

Friday, July 26, 2013

(Interview) DJ CHOKA ASEMA HANA UWEZO WA KUANDIKA MISTARI MIKALI ILA AKITOKEA MSANII WA KUMCHOREA NGOMA KALI ATAFLOW KWENYE BEAT MWENYEWE

DJ CHOKA Tumepiga Interview na DJ Choka a.k.a Mr Apetite ambapo kikubwa kilikuwa kuizungumzia Ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Latino Nation. Dj Choka amefunguka mengi kuhusu ngoma hiyo ambayo ni track yake ya 3 Kama Project zake ambapo ya kwanza ilikuwa Pamoja We Can ya Pili ikawa Press Play na hii ndo inaitwa Latino Nation.
tulitaka kujua kwanza kwa nini ngoma zake anafanya na Wasanii wale wale wa B Hits ambapo alipata kufunguka kuwa sababu kubwa ni kwamba bado anatamani kufanya na wale wasanii kwani kwanza yuko karibu nao zaidi pale Studio na kwamba mkataba wake wa Pale BHits Unamfanya pia atamani kufanya na Wasanii wa pale pale kwani Pia ni heshima moja wapo kwao.
Hata hivyo jamaa amepata kutujibu swali letu kuwa hataki kufanya ngoma na wasanii wengine ambapo alijibu kuwa Verry soon anafanya ngoma na Wasanii wengine haswa kafunguka kuwa anatamani kufanya collabo na Wasanii wakali wa HipHop toka Arusha.
Tulipozungumzia issue ya yeye kama hawezi kufanya ngoma yake mwenyewe akachora Mistari na Kuchana juu ya beat mwenyewe kuliko Kutafuta wasanii na kuwaweka wao katika Project yake Jamaa amefunguka na kusema kuwa hajawahi kufikiria hivyo kwani yeye hana uwezo wa Kuandika Mistari Concious ila kama atatokea Msanii atakayemuandikia Mistari atakayoikubali basi yeye yuko tayari kuflow kwenye beat kwani ana uwezo wa kutambaa na Beat ukizingatia kuwa anawapa Backup sana wasanii wengi kwenye show zao anazosimama kama DJ.
Kuhusu Heshima anayopewa na Watanzania DJ Choka amesema kikubwa anachokizingatia katika maisha yake ya kila siku ni kumuheshim kila mmoja awe mdogo au Mkubwa na akimuona mtu ni tatizo kwake yeye huwa anamkimbia huyo mtu.
HII HAPA CHINI NI INTERVIEW YAKE NA DJ HAAZU, MAY & VAY LEMA ON MJ RADIO 93.0 FM ARUSHA......
STORY BY DJ HAAZU.

1 comment:

Anonymous said...

kwani lazima nawewe urap?....watu kudevelop style ni talent na dedication iliyochukua muda mrefu hadi kumaster!...sasa we dj choka kazi yako ni u deejay ,,,kuhype kwenye ngoma na vitu ka izo mambo za kurap waachie wenyewe