22.11.13

Wednesday, July 24, 2013

(News) WASHINDI WATANO WAIBUKA NA MILIONI 10 KWENYE KWENYE PROMOSHENI YA"Cheka Plus"

 Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akimuonesha Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein namba ya simu ya mmoja ya washindi watano wa shilingi Milioni mbili wa Promosheni ya Cheka Plus.Kulia Samson Mwongela wa Idara ya Masoko Vodacom.
Vodacom Tanzania Public Relations Manager, Matina Nkurlu (left) displays a phone number to Hamud Abdulhuseein, an officer from Tanzania Gaming Board, when conducting Vodacom's Cheka Plus monthly draw. A total of five Vodacom customers won Tsh2 million each during the draw, looking on left is Samson Mwongela from Vodacom Marketing Department.

 Meneja Uhusiano wa Umma Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akimuonesha Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein namba ya simu ya mmoja ya washindi watano wa shilingi Milioni mbili wa Promosheni ya Cheka Plus kwa ajili ya uhakiki.
Vodacom Tanzania Public Relations Manager, Matina Nkurlu (left) displays a phone number to Hamud Abdulhuseein, an officer from Tanzania Gaming Board, when conducting Vodacom's Cheka Plus monthly draw. A total of five Vodacom customers won Tsh2 million each during the draw.

 Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akimshuhudia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na mmoja wa washindi wa Promosheni ya Cheka Plus ambapo washindi watano walijishindia shilingi milioni mbilimbili kila mmoja kupitia  Promosheni hiyo kubwa ya mwezi.
Hamud Abdulssein, an officer from Tanzania Gaming Board, looks on as Vodacom Tanzania Public Relations Manager, Matina Nkurlu (left) speaks on phone to one of the five winners who won a cash prize of Tsh2 million each through the company's Cheka Plus monthly draw. 

Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi watano wa Sh Milioni Mbili wa promosheni ya Cheka Plus kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa  Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.Promosheni hiyo inaendeshwa kila mwezi na Vodacom.
Hamud Abdulssein, an officer from Tanzania Gaming Board (right) confirms the phone number of one of the 5 winners who walked away with a cash prize of Tshs 2 million each through the Cheka Plus promotion,Left Vodacom Tanzania Public Relations Manager, Matina Nkurlu. 

Washindi watano waibuka na Milioni 10 kwenye Promosheni ya 'Cheka Plus'
*    Kila mmoja ajizolea Milioni 2
Dar es Salaam, Julai 24, 2013 ...Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 10 kupitia promosheni ya 'Cheka Plus.'
Kitita hicho cha Shilingi Milioni 10 kimenyakuliwa na washindi watano (5) ambapo kila mmoja amejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 2 kila mmoja kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus' iliyofanyika tarehe 20 mwezi huu.
Washindi hao ni pamoja na; Musa Hussein Ellmy ambaye ni mkazi wa (Karatu - Arusha), Vumi Joshua Mteru (Kilimanjaro), Joseph Godfrey Kyando (Tunduma, Mbeya), Anatori Emmanuel Chogolo (Dar es Salaam), na Amina Joseph Mmbaga (Arusha).
Meneja Uhusiano wa Umma wa Kampuni hiyo Bw. Matina Nkurlu, alisema kuwa zaidi ya wateja 6,000 wamefaidika na ofa hiyo kabambe inayoendelea hivi sasa nchi nzima ambapo zaidi ya Shilingi Milioni 100 zilikabidhiwa kwa wateja mbalimbali walioshinda kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus.'
Nkurlu alisema kuwa hadi hivi sasa, tayari wateja mbalimbali nchini wameweza kujishindia kiasi kinachofikia zaidi ya Shilingi milioni 100 "Tumekuwa tukipata washindi 100 kila siku ambapo wamekuwa wakijishindia shilingi 10,000 kila mmoja na washindi wengine 10 wakijinyakulia shilingi 50,000 kila siku, sambamba na droo kubwa ya mwezi ambapo katika washindi watano(5) kila mmoja wao amekuwa akijinyakulia  kitita  cha shilingi milioni mbili.
Hivyo toka uzinduzi wa promosheni hii ya 'Cheka Plus,' wateja takribani 10 wameweza kujishindia kiasi cha shilingi milioni mbili mbili kila  mwezi," alisema Nkurlu nakuongeza kuwa "promosheni hiyo  bado inaendelea hivyo ninapenda kuwasihi wateja wa mtandao wa Vodacom kuendelea kufaidika na huduma zetu ikiwemo promosheni ya "Cheka Plus" na kuweza kujishindia zawadi kemkem sambamba na kuendelea kuwasiliana na wapendwa wao."
Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa Promosheni ya 'Cheka Plus,' umewezesha wateja kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS), na kuperuzi kwenye mtandao wa intaneti bila hofu.
Ili kuweza kujiunga na huduma ya Cheka Plus, wateja wanashauriwa kupiga *149*01 # na kuchagua kifurushi wanachokitaka.
Promosheni ya Cheka Plus inawezesha wateja kutuma SMS na kupiga simu katika kiwango cha bei nafuu kabisa.
MWISHO.

No comments: