22.11.13

Monday, August 26, 2013

(News) VODACOM YAZINDUA DUKA LA 68 NCHINI

 Mkuu  wa Idara ya Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Bi.Upendo  Richard akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom lililoko kigogo Dar es Salaam,duka hilo linafikisha  idadi ya maduka 68 yanayotoa huduma kwa wateja nchini. Pamoja nae katika picha ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Bw.Matina Nkurlu(kulia) na kushoto ni Meneja wa Duka hilo Salum Chilala.

 Mkuu  wa Idara ya Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Bi. Upendo  Richard(katikati) akimkabidhi funguo Meneja  wa duka jipya la Vodacom lililopo Kigogo Dar es Salaam Salum Chilala, mara baada ya uzinduzi rasmi wa duka hilo linalofikisha idadi ya maduka 68 yanayotoa huduma kwa wateja nchini.Anaeshuhudia kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Bw. Matina Nkurlu.

 Meneja wa  duka jipya la Vodacom lililoko kigogo jijini Dar es Salaam Bw. Salum Chilala. Akifungua mlango kuashiria kuanza kwa huduma katika duka hilo mara baada ya kunduziliwa na Mkuu  wa Idara ya Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Bi. Upendo Richard(katikati) Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Bw. Matina Nkurlu.

Mfanyakazi wa duka jipya la Vodacom lililoko kigogo jijini Dar es Salaam, Meshack Mgana akiuunganishia intaneti kwa  moja ya wateja waliojitokeza kupata huduma katika duka hilo, Bw. William Mwakalwasya  Duka hilo linafikisha  idadi ya maduka 68 yanayotoa huduma kwa wateja nchini.

No comments: