22.11.13

Friday, September 06, 2013

WALTER CHILAMBO AKIRI KWAMBA MWAKA HUU WALIOJITOKEZA EBSS HAWANA UWEZO KAMA WA MWAKA JANA

DJ HAAZU NA WALTER CHILAMBO 

Mshindi wa Million 50 za EBSS mwaka jana na HitMaker wa Siachi na Doro "Walter chilambo" amefunguka exclussive kwenye Interview na DJ HAAZU wa MJ FM Arusha na kusema kwamba waliojitokeza kuingia katika kinyang'anyiro cha EBSS mwaka huu hawakuwa na hamasa kama Mwaka jana.
Walter amesema kwanza hata idadi ya washiriki waliokuwa wakijitokeza katika Mchujo kwa kila Mkoa haikuwa kubwa ukilinganisha na Mwaka Jana ambapo Idadi ilikuwa kubwa kitu ambacho anasema Mwanzoni tu kupitia Usaili alianza kusanuka kuwa kama kuna Udoro flani ukilinganisha na Mwaka jana.

Yeye mwenyewe binafsi anasema hajajua ni kwanini lakini kikubwa ni kwamba hata wale ambao wameingia Top 20 hawana yale mashamsham kama ya mwaka jana jana japo wana uwezo lakini anaamini kwa kuwa wanaingia kambini wataiva muda si mrefu kwani kule watapata nafasi pia ya kunolewa na kutolewa ubutu walionao.
MSIKILIZE CHILAMBO HAPA CHINI AKIFUNGUKA

CLICK LINK HII KUMSIKILIZA http://www.hulkshare.com/x6pyy1iv6lmo
Kwa upande mwingine Walter amepata kufurahishwa pia na uwezo wa wasicha waliojitokeza kwa mwaka ambapo pia katika Idadi hiyo ya top 20 Wasichana ni wengi kuliko Wavulana tofauti na Miaka Mingine

HAPA CHINI MSIKILIZE TENAAKIZUNGUMZIA UWEZO WA WASICHANA MWAKA HUU

CLICK LINK HII KUMSIKILIZA http://www.hulkshare.com/yrr1kog0vk74

HABARI NA DJ HAAZU

1 comment:

Eazzy Khameed said...

Bro, Umefua mbna hata wewe hauna uwezo wowote!