22.11.13

Monday, September 28, 2009

SHOW YA FIESTA ONE LOVE DODOMA. (JAMUHURI STADIUM)




Msanii Cyrill alijitaidi kufanya show nzuri na kuitawala steji akiwa na mwenzake.

dj choka alikuwa akiwapigia wasanii wote waliokuwepo kwenye fiesta Dodoma.

Izzo biznes nae ilifikia wakati wake akapanda jukwaani na kukimbiza kama kawa.

Kule kushoto ni Madee na Tunda man, madee aliwanyanyua raia wa dodoma na wakatoka walikokuwa na kusogea mbele kabisa, walipata shangwe nyingi sana.

Mzee wa fasta Quick racka nae hakuichezea bahati yake kwa kupiga show nzuri.

Watoto wa Zanzibar Samaki samaki walipiga mduara wa nguvu kwa wakazi wa dodoma, na siku hiyo samaki aliliwa jicho kweli.

P.Square wa bongo Jonson & Jackson walikamua vilivyo

Mtoto wa nyumbani Mez B wa Area C aka Melody alifanya vizuri nae ingawa hakupata shangwe ki hivyo.

Mtoto wa Tanga Suma Lee akiwa kwenye jukwaa la Fiesta akikamilisha ratiba.

Sumu ya penzi ndio iliyomfanya Bellenine kufanya show nzuri na kumgusa kila mmoja.

Hapa kwa kweli hata mimi sijaelewa, dereva wetu juma wa pili kutoka kushoto alikuwa anawaambia wenzake eti nani mweupe kuliko mwenzake.

Niki wa 2 mdogo wake Joh Makini aliiwakilisha River Camp kwa wakazi wa dom

Mzee wa style 3 tofauti anajulikana kwa jina la Stopa wa rhymes

Watoto wa Tmk Family Chege na mwenzake stiko waliwakilisha ipasavyo

Mr. Blue na Hamidu walionyesha vitu vizuri na wakaichezea steji ipasavyo.

Nahisi mnaiona steji ilivyo na mnaona huo umati hapo mbele, sasa nyuma yangu ya camera ilikuwa mara mbili ya hao hapo chini.

Jioni ilianza kuingia na camera yangu ilianza kuisha chaji, stejini pale ni Chidi Beenz pamoja na La familia...
Wengine waliopanda ni Prof Jay, Fid Q, Juma Nature na wengine wengi, camera yangu iliisha chaji nikashindwa kupata matukio.

No comments: