22.11.13

Wednesday, November 18, 2009

SHOW YA FIESTA ONE LOVE ZANZIBAR.

Show ya Fiesta One love kwa upande wa ZNZ ilifanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe, wasanii walipendeza sana na walifanya show safi sana. Naomba radhi kwa picha kuwa chache za show kwasababu camera yangu ilikata chaji na nikawa sina ujanja zaidi.
Hapo juu ni msanii mkali kutoka Morogoro anaitwa Belle 9.

Ally Kiba alitoka bomba sana huku akiwaimbia wazanzibar kwamba wasimcheke akiwa anapenda kula.

Kijana kutoka Clouds TV akiwa anachukua matukio kwa umakini zaidi.

Washkaji wakiwa wamekula pozi wakitizama show

Vijana kutoka TIP TOP wakikamua stejini, Kushoto ni Tundaman na Madee

Wasanii wanaipeperusha bendera ya ZNZ wanajulikana kwa jina la Offside sijui nini....mimi nawajua kwa jina la Samaki Samaki, yaani Samaki mweusi na Samaki mweupe ha aha ha
walipiga mduara wa nguvu na hakuna aliyekaa chini.

Wasanii wengine waliopanda ni Mangwear, Fid Q, Chidi Beenz Baby J, Pasha, Chege na kundi lake la TMK.

No comments: