22.11.13

Friday, December 18, 2009

NILISHIKA MAWILI NASHUKURU MUNGU HAKUNA LILILONIPONYOKA.

Anaitwa Black Rhino aka The Dandada, mtoto anayetokea kwenye familia yenye akili nyingi sana nikimaanisha familia ya mzee Haule. Juzi tarehe 11 mwezi huu Black Rhino ilikuwa ni Graduation yake pale Chuo kikuu cha Mzumbe(Morogoro).
Alikuwa anatunikiwa Degree ya Biashara na Masoko yaani BACHELOR OF BUSINESS ADMINISTRATION IN MARKETING MANAGEMENT. Ilikuwa ni furaha na nderemo kwenye familia hiyo, namnukuu
"Dj Choka namshukuru mungu kwani nilikuwa na wakati mgumu wa kufanya mziki huku nasoma, ila nilivumilia na nikaweza kupigana nayo, na sasa ninadegree yangu."

Baba mzazi wa Black Rhino mzee Haule akiwa na mwanae nyumbani kwake Mikumi.

Rafiki mkubwa wa Black Rhino Dativa Mango akiwa anampa hongera zake.

Kushoto ni Girlfriend wa Black Rhino, katikati ni mdogo wa mwisho wa mzee Haule anaitwa Kolihombi.

Shemeji, dada wa black rhino(Viola), katikati ni mama mzazi wa Rhino na pembeni ni braza naniliii..

HONGERA SANA BRO.

1 comment:

Anonymous said...

Nimefurahi kumuona dada viola huyu nae alikuwa anaimba sana enzi hizo tunasoma morogoro

miaka inakwenda kweli duh!!